Ripoti: Android P itakuwa na muonekano wa iPhone X

Mwandishi Alexander Nkwabi

Mpaka sasa sio simu nyingi tayari zimepata sasisho la toleo jipya mfumo endeshi wa Android Oreo. Na tayari Google wanajiandaa kuachia toleo linalofuata la mfumo endeshi huo ambao kwa sasa umepewa jina la Android P. Mpaka muda huu Google hawajatoa taarifa zozote rasmi kuhusu jina au vitu vitakavyo ongezwa au kupunguzwa kwenye toleo hili jipya. Hata hivyo tayari kuna tetesi tayari zimeanza kuzagaa mtandaoni kuhusu sasisho hili.

Chanzo ambacho hakikupenda kutaja jina lake, kimevujisha taarifa kuhusiana na toleo jipya la Android P, akiongea na Bloomberg, chanzo hicho kimeelezea muonekano wa Android P umesukumwa na muonekano wa iPhone X hasa kile ki “notch” upande wa juu kioo ambacho Samsung walikitumia kuwapiga dongo Apple.

iphone-notch

Chanzo hicho kiliongeza, Sasisho hili  la Android pia litatia mkazo kwenye program ya Google Assistant, kuboresha maisha wa betri, na pia kuweza ku support simu zenye vioo zaidi ya kimoja na zile zenye vioo vya kujikunja.

Google wamejikita zaidi katika kuwavuta watumiaji wa iPhone warudi kutumia mfumo wa Android na ndio maana sasisho hili linaongeza vitu hivyo. Msemaji mkuu wa Google hakukubali au kukataa madai ya mvujishaji huyu.

Hatutegemei kampuni ya kutengeza simu ya Samsung kutoa simu yenye “notch” maana wameonekana kutopenda feature hiyo pale walipowadhihaki kwenye tangazo lao la galaxy s8. Hata ivyo kuna simu kama Essential phone tayari zimekuwa na notch hapo kabla.

GoLcDRC

Endelea kuwa nasi kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii ili usipitwe na Habari, Uchambuzi na Makala mbali mbali za kiteknolojia kwenye FacebookTwitterInstagram, Google+ na Youtube, Pia usisite kutoa maoni yako hapo chini au tuandikie barua pepe kwa mhariri@mtaawasaba.com

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive