Samsung Galaxy Fold: Kwanini usubiri toleo linalofuata

Simu-Tableti yenye kioo cha kujikunja ya Samsung Galaxy Fold hatimaye imezinduliwa kwenye tukio la Galaxy unpack pamoja na simu za familia ya Galaxy S10, hii ni baada ya miaka ya kusubiri na tetesi kibao kuhusu simu hii. Ili uweze kuimiliki simu hii ni lazima toboke mfuko maana bei yake ni dola za kimarekani takribani 1980 sawa na shilingi za kitanzania 4,642,000 hivi.

Bidhaa nyingi hasa za kiteknolojia zinapotoka toleo la kwanza mara nyingi zinakuwa na matatizo mengi hata kama zitafanya mapinduzi ya kiteknolojia. Ukiangalia iPhone, iPad, Microsoft Surface n.k matoleo ya kwanza yalifanya mapinduzi makubwa japo hayakuwa vile tunavotamani iwe.

Hebu kwa haraka haraka tupitie mambo mazuri ambayo Samsung Galaxy Fold imefanikiwa.

fold-multiple

Muonekano wa simu hii ni mzuri, wa kawaida na wa kipekee kabisa (mpaka sasa aliyetengeneza kama hivi). Hapa Samsung wamekuwa wa kwanza kama ilivokuwa kwenye Phableti.

Kioo cha Galaxy Fold, kina ukubwa wa inchi 4.3 inapokuwa imekunjwa na inchi 7.3 inapokuwa imefunguliwa.

Kwa upande wa sifa:

 • Ukubwa wa kioo: 4.6-inch Super AMOLED; 7.3-inch QXGA+ Dynamic AMOLED
 • Mfumo endeshi: Android 9.0 with Samsung One UI
 • Kamera: 16-megapixel (ultra-wide-angle), 12-megapixel (wide-angle), 12-megapixel (telephoto)
 • Kamera upande wa mbele: Two 10-megapixel, 8-megapixel 3D depth
 • Prosesa: Octa-core Qualcomm Snapdragon 855
 • Hifadhi: 512GB
 • RAM: 12GB
 • Memori kadi: None
 • Betri: 4,380 mAh
 • Fingerprint sensa: upande wa kulia

Simu hii inakuja na jumla ya kamera sita, ndio kamera sita kwa ujumla, hifadhi ya gb 512 kioo cha kupendeza cha AMOLED.

Kwanini usubiri toleo lijalo

Hatusemi kama Samsung wamefeli, ila hivi ni vitu ambavyo kama vitafnyiwa maboresho, basi simu hii itakuwa iliyoleta mapinduzi kwa siku za baadae.

 • Ni nene sana kiumbo na haivutii kimuonekano
 • Mfumo endeshi kwenye simu hii bado hauko vizuri
 • Kioo cha inchi 7.3 hakina tofauti kubwa na kioo cha inchi 6.5
 • Bei yake ni kubwa kupita kiasi kwa kifaa cha toleo la kwanza
 • Walengwa wa simu hii kwa sasa ni wale wanaopenda kujaribu teknolojia mpya, na wenye fedha zisizo za mawazo.
WAWEZA SOMA:  Huawei wazindua HarmonyOS, mfumo endeshi kwa ajili ya vifaa janja

Kwa kifaa kinachotoka kama toleo la kwanza, Samsung tunawapa hongera kwa uthubutu wa kuja na kifaa chenye sifa za kipekee kuliko chochote kwene soko kwa sasa. Kama mjuavyo watakaofuata wote kutengeneza simu za kujikuja watasemwa wamenakili kutoka Samsung, hasa Apple ambapo tayari inasemekana anaweza pia kutoa simu/kifaa kinachojikunja pia.

Kama nilivoandika huko juu jinsi nilivopenda uthubutu wa Samsung kuleta kifaa hiki, ila nadhani ni vyema tukisubiri Galaxy Fold 2 kwa ajili ya maboresho zaidi.

 

HAKUNA MAONI

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa