Sharp wazindua simu janja ya kwanza yenye notch mbili

Mpaka sasa watengenezaji wa simu wanatafuta namna ya kupunguza ukubwa wa notch kwenye simu janja mpya zinazotarajia kutoka pia ni pamoja na kuhamia kwenye miundo itakayowezesha kuondoa notch kabisa kwenye kioo.

Katika hali ya kushangaza kampuni ya simu za mkononi ya Sharp imezindua simu yenye notch mbili, simu hiyo iliyopewa jina la AQUOS R2 compact inakuja na sifa kedekede.

Watumiaji wengi wa simu za mkononi wameonekana kutofurahishwa na notch kwenye kioo, lakini hilo halikuwazuia Sharp kutoa simu hiyo yenye notch mbili, juu ya kioo na chini na kuifanya simu hhiyo kuwa ya kwanza duniani ya namna hiyo

Simu hii ya SHARP AQUOS R2 compact inatarajiwa kuuzwa kwenye soko la Japan, mpaka sasa haijajulikana kama watengenezaji wengine wa simu watafauata mkondo huu wa kutoa simu zenye notch juu na chini ya kioo baada ya kuanza kuonekana hazivutii na kuamua kugeukia teknolojia zingine.

Notch ya upande wa juu inafanana kwa ukaribu na ile iliyo kwenye Essential Phone na ina kamera ya selfie, wakati notch ya chini ina sensa kwa ajili ya fingerprint, kwa ujumla ukubwa wa kioo ni inchi 5.2 ambazo kwa sasa inaonekana ni kioo kidogo.

Usikose Kusoma:  Nokia 8110 yarudi ikiwa na 4G, Facebook na kifuniko cha Matrix

Baadhi ya sifa za simu hii ni pamoja na kioo cha LCD chenye ukubwa wa pikseli 2280 × 1080 na refresh rate of 120Hz. Simu hii inakuja na prosesa ya Snapdragon 845, RAM yenye GB4 na ukubwa wa GB64, simu hii ina mfumo endeshi wa Android 9 Pie na betri yenye uwezo wa 2500mAh.

Leave a Reply