Simu pekee kwa ajili ya makundi maalum katika jamii

Mwandishi Hemedans Nassor

ni kawaida kuona watu muda wote wakizungumzia makampuni makubwa ya simu kama apple na samsung wakati wanapotaka kuchagua simu na kusahau simu wanayohitaji ni ya aina gani. leo nimejaribu kuonesha aina za simu ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya makundi pekee katika jamii.

 

simu za wazee

hebu fikiria una baba, babu, bibi, mama au mtu yoyote kwenu ambaye umri wake ni mkubwa na unataka umnunulie simu je utamnunulia simu kama samsung na iphone? jibu ni hapana maana hazijatengenezwa zitumiwe na watu kama hawa. zipo simu ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya wazee tu zipo nyingi ila mimi nitataja moja tu kama sample kuonesha simu ya wazee inatakiwa iweje.

 

fujitsu stylistic s01

Stylistic

 

kama inavyoonekana kwenye picha hii ni simu ya android iliyocopy muonekano kama wa windows phone kuifanya simu iwe na mambo muhimu pekee kwenye screen. wazee huwa wanapenda mambo machache kama kupiga simu na message.

 

specification za simu sio kubwa saaana kusema zitakushangaza ni za kawaida zitakazofanya simu kuoperate vizuri.

  • kioo 4 inches
  • Android 4.0 Ice Cream Sandwich ndio operating system yake
  • 1.4GHz Qualcomm processor ikiwa na  512MB ya RAM
  • 8.1 MP camera ya nyuma na  0.3MP camera ya mbele
  • 4GB  ya internal memory na inakubali memory card

 

 

smartphone ya wanokaa maeneo yasiyo na umeme au wanataka simu ya kukaa sana na charge.

 

hii simu ni nzuri kwa charge inakaa na charge zaidi ya wiki lakini ili kufikia lengo hilo wamefanya sacrifice kubwa kwa kutoa kioo cha rangi na kueka e lnk screen ambacho ni kioo kinachoonesha rangi nyeupe na nyeusi tu.

Eink-3Eink-4

 

japo ina kioo kisicho na rangi simu hii iiliyotengenezwa na kampuni ya makaratasi (siunaona ipo kama gazeti) inatumia operating system ya android na kuifanya iwe powerfull kama smartphone nyengine tu. mfano kwa simu hii utaweza ongea skype, viber na tango.

Fndroid02Fndroid01

 

nayo hii haina specific za kutisha maana haihitaji power, na pia ina weakness nyengine ya kutosuport video. haijaingia madukan bado ila bei itakua chini ya laki 3 kuna version ya 3g na ya edge.

 

simu za maeneo yenye usalama mdogo kama jeshini na wakandarasi

hebu fikiria we ni mwanajeshi au wewe ni fundi wa ujenzi upo maeneo hatari hatari then unakua na simu laini laini lazima itapunguza ufanyaji kazi wako maana mda wote unaogopa kuidondosha. siku hizi kuna simu zimetengenezwa kuvumilia maisha magumu (rugged phone) hizi ni simu ambazo ukidondosha au kudumbukiza kwenye maji haupati hofu yoyote. hapa pia ntataja moja kuonesha mfano wake.

 

 

Caterpillar CAT B15

Caterpillar-b15-rugged-android

 

kama unavyoiona simu imekaa kikazi kazi kweli ikiwa na vyuma na rubber kwa pembeni simu hii inavumilia kudondoshwa umbali wa futi 6 na inakaaa kwenye maji hadi dakika 30. pia simu hii inafaa mazingira ya baridi na joto na haitadhurika kwa baridi kali wala joto jingi. inatumia operating system ya android jelly bean na ina ram ya 512mb na processor dual core cortex 1ghz.

bei ni around laki 7

Avatar of hemedans nassor
Mwandishi Hemedans Nassor Mchangiaji
Hemedans aka Chief Mkwawa, amekuwa mwandishi wa makala mbalimbali za teknolojia kuanzia kuanzishwa kwa Mtaawasaba. Kwa sasa ni mchangiaji kila anapopata nafasi
2 Comments

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive