Blog smart kwa kutumia Microsoft word

Kuna watu wengi wanamiliki blogs Tanzania lakini hawana uwezo wa kucode na kusababisha kupata shida sana wanapotaka kucostomize post za blog ziwe kama wanavyotaka wao. Lakini watu hao hao unakuta ana uwezo mkubwa tu wa kutumia Microsoft word. Leo nitawaelekeza namna ya kuitumia Microsoft word kupost kwenye blog yako. Njia hii itawanufaisha wanoblog kwa blogspot na wordpress.

 

Vitu vilivyomo kwenye Microsoft word vitakavyokunufaisha

  1. Uwezo wa kuangalia homepage ya blog yako kupitia Microsoft word (itafungua kwa browser)
  2. Unaweza kuieka post ya blog yako katika category yoyote uliyotengeneza kupitia Microsoft word
  3. Unaweza kuedit post ya zamani kupitia Microsoft word
  4. Unaweza kueka account mbali mbali kwenye Microsoft word yako kwa ajili ya kublog
  5. Kupublish blog post kutokea Microsoft word
Usikose Kusoma:  Chromebook Pixel: Laptop ya kisasa ya google yazinduliwa

 

NJIA ZA KUFATA ILI KUWEZA KUBLOG NA MICROSOFT WORD

 

Step ya kwanza

Andika post yako kwenye Microsoft word kama unavyoandika kazi nyengine remba kadri unavyoweza, ukitaka weka picha idadi unayotaka hadi post ikamilike.

Step ya pili

Bonyeza file then bonyeza save and send then bonyeza publish as a blog post (hii ni kwa Microsoft word 2010) kwa wanaotumia Microsoft 2007 njia inaweza kua tofauti kidogo ila lengo ni moja.

 

Step ya tatu

Itafunguka sehemu nyengine click publish as a blog post

 

Step ya nne

Itafunguka sehemu ya blog eka title na kama unataka kuieka post kwenye category Fulani utaeka hapa, kama ni mara ya kwanza kutumia itabidi uset username na password ya acont yako ya blog hapa. Then utapublish 4

Usikose Kusoma:  FIFA waruhusu teknolojia ya video (VAR) kutumika kwenye Kombe la dunia 2018

 

JINSI YA KUSET USERNAME NA PASSWORD

Kama ni mara ya kwanza ukiclick publish itapop up sehemu ya kueka username na password lakini kama ni mtumiaji tayari click manage account then add.

Mara yako ya kwanza utaambiwa uchague provider wako wa blog. Kuna kina blogspot, wordpress, typepad, community server, sharepoint blog na windows live space. Utachagua kutokana na provider wa blog unaetumia. Mfano mimi nimechagua wordpress.

Hio sehemu nilipozungushia red utaeka url ya blog yako hapo utaondoa <enter your blog URL here > na utareplace url yako. Mfano mi na assume url yangu inaitwa blogyangu.wordpress.com

Then unaeka user na password ur done. Enjoy kublog.

 

kumbuka Picha zinakua uploaded automatic so usihofie na pia kama unataka kuadd feature image publish kama draft kwa ajili ya kuadd badae

3 MAONI

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa