HTC One – Jet Li wa smartphone

Hatimaye kampuni ya wataiwan htc wamezindua simu yao mpya kabisa ya htc one. Usichanganye jina na htc one x na one x+ hii ni simu mpya kabisa na bora kuliko simu zote za htc kupata tokea. kama utakua ni mfatiliaji mzuri wa simu mwezi huu wa pili ndio mwezi ambao mobile world congress inafanyika na pale barcelona tutaona simu nyingi toka nokia, lg na asus, pia mwezi march au april samsung galaxy s4 itazinduliwa simu zote hizo zitakua zinapambana na hiii htc.

htc-mtaawasaba htc one imeitwa jet li wa smartphone kwa ukubwa wa specification zake

 

SPECIFICATION ZA SIMU

Hii simu inatumia operating system ya android ikitumia latest version ya jellybean 4.1.2  na itakua na kioo cha 4.7 inch ambacho kina resolution ya 1080×1920. hii resolution ni full hd ndani ya kioo kidogo hivyo na kuifanya screen iwe na pixel 468 kila inch. kwa sasa hii ndio screen yenye quality nzuri zaidi. simu hii itatumia processor mpya kabisa ya qualcomm iitwayo snapdragon 600 ambayo ni quadcore (ina core 4) na yenye speed ya 1.7ghz, pamoja na hio processor simu hii itakua na ram 2gb. vitu vyengine ni kama camera ya 4mp na battery ya 2300mah.

Usikose Kusoma:  Nokia 9 PureView yenye kamera tano yazinduliwa kwenye maonesho ya MWC 2019

 

CAMERA YA SIMU

nitakua sijatenda haki kama ntaielezea hii simu bila kuielezea camera yake. simu hii itakua na camera ya 4megapixel(mp), whaaaaat 4mp? yes 4mp. najua utajiuliza why simu kubwa kama hii iwe na 4mp then jibu wanalo htc. hii technolojia htc wanaiita ultrapixel ni technolojia ambayo pixel ya kwenye picha inakuzwa na kua kubwa ili kuruhusu mwanga mwingi uwe kwenye picha na kuzifanya picha zitoke kwa quality kubwa. hii ni vice versa ya camera za nokia na iphone ambazo zinatumia oversampling technology kupata picha yenye quality nzuri.

camera-mtaawasabahtc wanasema camera yenye megapixel kubwa kuchangia quality ya picha ni BIG FAT LIE

pamoja na ultrapixel technology kuna kitu kinaitwa htc-zoe hii ni feature ya camera ya htc one ambayo itakuwezesha wewe mtumiaji kuweza kutengeneza mixing ya picha na video na kutoa vitu kama animation zenye effect nzuri. mfano unachukua video watu wawili wanatembea then mmoja hutaki atokee kwenye ile video yako then kupitia hii feature unaweza ukamtoa.

Usikose Kusoma:  Bitcoin: Yote unayohitaji kufahamu

 

HTC ONE DESIGN AND COLOR

mwanzo htc walisema simu hii itapatikana na rangi tatu, silver, nyeusi na nyekundu lakini habari zimechange kua simu hii itapatikana kwa rangi nyeusi na silver tu

red-htc-onehtc-one-big

 

kama unavyoiona simu itakua na muonekano kama wa iphone5 au blackberry z10 kwa mbele. ni nyembamba na sio nzito sana.

 

bei ya simu itakua around milion 1 na laki 2 za bongo hadi milion 1 na nusu

HITIMISHO LANGU NA USHAURI

kama wewe unapenda simu ya kisasa uende na fashion pamoja na simu ambayo ni powerfull itakayorun software na games zote za android then hii simu niyako. wale ambao pia wanapenda camera kujipiga picha na ku upload kwenye mitandao ya kijamii pia hii simu yako. lakini kama unapenda camera ya kuja kuprint baadae hii si simu yako kutokana na udogo wa megapixel

 

usisahau kuacha muono wako kuhusu habari hii hapo chini

2 MAONI

  1. ebwana daaah hii kitu ni revolutionary, ila ndugu mwandishi umeniacha hoi na “htc wanasema camera yenye megapixel kubwa kuchangia quality ya picha ni BIG FAT LIE”

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa