Piga simu bure kwa kutumia internet kwenye simu na pc yako

hapa nitajaribu kuwakusanyia application karibia zote zinazotumia network ya 3g (hata wifi yenye speed inafaa). hizi application zitakuwezesha kupiga simu bure na kukatwa hela ya internet tu. so kama una unlimited data ya internet uta enjoy. hizi application hazipigi bure kwenda kwenye simu za mikononi (tigo, vodacom.zantel na airtel) wala mezani (ttcl) bali ni bure pale yule unaempigia naye ana application kama yako. mfano mimi nina skype na wewe una skype tukipigiana ni bure.

Pia usihofu kuhusu hela ya internet itakayokatwa ni ndogo sana. Bundle ya mb50 ya extreme au cheka inaweza kuwezesha kuongea zaidi ya masaa matatu.

NIMBUZZ

nimbuzz ni social network maarufu ni inassupport kuchat, magame pamoja na kucall bure. ina faida moja ya kukubali kuingia kwenye device karibia zote. nimbuzz ipo kwenye simu pamoja na computer. Mfano wa aina za simu zinazokubali nimbuzz ni

  • JAVA- hizi ni simu kama nokia na Samsung zinazotumia java mara hzote hizi si smartphone na hufanya mambo machache kama vile nokia asha zote.
  • SYMBIAN- hizi ni nokia smartphone maarufu kama n series na eseries ukiona simu yoyote imeanza na N au E ya nokia jua inakubali nimbuzz
  • ANDROID- hizi ni simu kama Samsung galaxies, htc, lg za touch, sony na Huawei nazo zinakubali nimbuzz
  • IOS- iphone zote zinaingia nazo
  • BLACKBERRY- simu zote za blackberry
  • WINDOWS PHONE- nokia lumia, htc na Samsung ativs zote zinaingia nimbuzz
Usikose Kusoma:  Jinsi ya ku-secure switch yako ya cisco

Ukiangalia juu utaona karibia simu zote zinaingia nimbuzz hii inaifanya iwe maarufu sana katika client hizi za kupigia simu. Ili umpigie mtu simu na nimbuzz inabidi wote wawili muwe mumeidownload. Nimbuzz wana video call kwa pc na baadhi ya handset

Kudownload nimbuzz click hapa http://nimbuzz.com

SKYPE


hii ni kama nimbuzz sema haissuport java inakubali simu za symbian iphone(ios) android, blackberry na windows phone pia inakubali kwa pc. hii ina faida nyengine ya kukubali video calling. chakufanya ni wewe kuwa na skype na mwenzako kua nayo then unampigia na kuenjoy free call kuipata click link hapo chini

Usikose Kusoma:  Simu pekee kwa ajili ya makundi maalum katika jamii

http://skype.com

VIBER


Viber ni moja kati ya application maarufu kwa sasa kwa ajili ya kupiga simu za bure na hawa jamaa wanajitahidi kuifikisha application yao kwenye kila pembe ya dunia hadi visimu vidogo vya asha sasa vininaingia viber. Viber ipo pia kwenye blackberry, iphone, simu zote za android, windows phone zote na Symbian kuipata click link hapo chini

http://viber.com/

TANGO


Tango wao hawapo interested na simu ndogo focus yao ipo kwenye smartphone tu na kwa sasa wanapatikana kwenye iphone, ipad, simu zote za android, windows phone na pia wanapatikana kwenye pc na laptop. Ukiwa na tango utapiga call buree na video call pia kuidownload click link hapo chini

http://tango.me

FRINGE


Hawa jamaa si kukubali calls tu bali pia wana video call wanakubali wao wanapatikana kwenye Symbian, androids na iphone. Kuidownload hapo chini click

http://fring.com

kama una swali lolote usisite kuuliza chini

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa