Simu isiyoingia maji ya Sony Xperia Z

Habari njema kwa watu wote, kampuni ya sony wamezindua simu isiyoingia maji, simu iliyopewa jina la XperiaZ inaweza kuzamishwa mpaka futi 3 chini ya maji kwa muda wa mpaka nusu saa bila kuharibika

Usikose Kusoma:  Blog smart kwa kutumia Microsoft word

Watengenezaji wake waliijaribu bafuni, simu zingine kama iphone huaribika haraka iwapo zitaingia maji au kudondoshwa. Sony’s Xperia Z imefunikwa kwa kioo kinachokunjika na kuzuia kuvunjika, lakini chembamba kwa milimita 7.9
simu hiyo ilizinduliwa kwenye Consumer Electronics Show (CES) huko Las Vegas,

simu hiyo pia ina kamera ya hali ya juu yenye – 13 megapixels, yenye nguvu kuliko ile ya iPhone 5 ambayo ni 8 megapixel pekee.

Usikose Kusoma:  Siri ya TECNO kuongoza zaidi ya Asilimia 50% kuuza bidhaa nyingi Tanzania.

simu hiyo inayotumia android, ina uwezo kuongeza maisha ya betri kwa kuzima programu zisikuwa na umuhimu kwa wakati huo.
pia ina mfumo wa intanet wa 4G connection,na inchi 5 Full HD 1080p.

2 MAONI

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa