Yahoo imenunua application iliyotengenezwa na Kijana mwenye umri wa miaka 17 kwa mamilioni ya dola

Ni mbunifu wa app ya habari iitwayo ‘Summly’, kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 amejikuta amekuwa milionea baada ya Yahoo kuinunua application yake.

Japo haijulikani ni kiasi gani hasa alicholipwa lakini ni mamalioni ya dola.App hiyo itaanza kutumika kwenye products za Yahoo. Summly huchukua habari za mtandaoni na kuzifupisha kuwa na maneno 400 ambazo ni rahisi kusomwa kwenye simu za mkononi.

Usikose Kusoma:  Google Play Store sasa itawawezesha kujaribu programu kabla ya kuzipakua

Pia, mtoto huyo atakuwa mwajiriwa wa Yahoo mwenye umri mdogo zaidi.Nick aliitengeneza app hiyo akiwa na umri wa miaka 25 na kupata uwekezaji kutoka kwa kampuni ya bilionea wa Hong Kong, Li Ka Shing iitwayo Horizons Ventures na kupata shavu kutoka kwa mastaa kama Stephen Fry, Yoko Ono na Ashton Kutcher waliowekeza kwa zaidi ya paundi milioni moja.

Usikose Kusoma:  Instagram yazindua IGTV, programu tumishi kwa ajili ya video ndefu.

App hiyo kwaajili ya simu za iPhone ilianzishwa December 2012 na Summly ilifanya kazi na mitandao zaidi ya 250 duniani.

Maoni 1

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa