Ni masaa kadhaa yamebakia kabla Apple hawajaanza tukio lao kubwa kabisa maarufu kama Apple event 2021 ambalo mwaka huu wamelibatiza jina “California Streaming”, linatarajiwa kuanza saa mbili usiku siku ya jumanne Septemba 14, ambapo tunatarajia watazindua bidhaa kadhaa ikiwemo iPhone 13, mfululizo wa Saa janja za Apple Watch 7 na pia wanaweza kuachia Airpods 3. Japo mpaka muda huu hatuna uhakika mpaka tukio litakapoanza rasmi iyo usiku.