Facebook kuondoa kipengele cha Trending Topics hivi karibuni

 

Facebook imeamua kuondoa kipengele cha Trending topics, habari imeandikwa kwenye blog ya mtandao huo wa kijamii wa Facebook. Kipengele icho cha Trending topics kilianzishwa mwaka 2014, mahususi kwa ajili ya kusaidia watu kupata taarifa ya mambo yanayovuma kwa wakati husika.

Kipengele hiki kilileta mtafaruku mkubwa mnamo mwaka 2016 baada ya mtandao wa Gizmodo kutoa taarifa kuwa kuna watu wameajiriwa kuhakikisha nini kinaonekana na nini hakionekani kwenye kipengele hicho. Baada ya taarifa hiyo ilibidi timu zima ifutwe kazi na kuanzia hapo kipengele icho kinategemea algorithim ili kuonesha habari au taarifa ya mambo yanayovuma.

Usikose Kusoma:  OnePlus 5T: Unahitaji simu hii kwa matumizi zaidi ya simu

Sababu kubwa kuondoa kipengele hiki ni kuwa haionekani kwa na watu wengi. Akizungumza bwana Alex Hardiman, ambae ni mkuu wa habari, amesema kipengele icho kinachoonekana nchi tano tu, ni asilimia 1.5 tu ya watumiaji ndio imekuwa ikitembelea kipengelea icho.

Facebook inaondoa kipengele hiki ila inasisitiza kuwa inaangalia namna ya kukuletea njia zingine mbadala na rahisi kutumia ili uweze kupata habari za taarifa zinazovuma kwa wakati.

Usikose Kusoma:  Vitu 6 vilivyogunduliwa na wanawake na kubadili dunia

 

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa