Maonesho ya CES huko laa vegas yanaendelea, Katika pita pita mtaawasaba imekutana na kifaa kinachokuwezesha kufanya mazungumzo yako ya kibinafsi hata ukiwa katika mkusanyiko wa watu wengi.
Kifaa hiki nimaalumu kwa kukivaa usoni pale unapohitaji kufanya mazungumzo yako ya kibinafsi. Ikiwa uko mgahawani, kwenye basi kama la mwendo kasi au sehemu yoyote ya wazi kifaa hiki kitakusaodia kufanya mazungumzo na mpendwa wako bila yeye kusikia kelel zozote zinazoendelea maeneo hayo.