Ushindani: Simu za Tecno Vs Infinix

Mwandishi Diana Benedict

Tecno iliingia soko la Africa ili kutoa Smartphone za bei nafuu kushindana na bidhaa maarufu kama Samsung, LG, na HTC tangu mwaka wa 2013, kampuni hiyo ilianza kutoa vifaa vya hali ya kati ambavyo vinaweza kutumika katika soko la Africa hasa Tanzania kwa ufanisi.
Infinix kwa upande mwingine inalenga kuharibu soko la bidhaa za kati na la chini na soko la smartphones bora. Kampuni hiyo ilifafanua nini maana ya smartphones za bajeti za chini na za kati baada ya kuanza kwa Africa hasa Kenya na Tanzania kwa kuzindua Infinix Hot Note na Infinix Hotx507.
Katika sekta ya smartphone, ushindani na chuki umekuwepo katika simu za Samsung na simu za Apple; Android vs iOS. Ushindani umekuwa katika bodi, Camera na Tecknlojia tofauti tofauti. Katika Africa hasa Tanzania kuna mapigano ya polepole katika simu za Infinix na simu za Tecno, na kwa hakika katika hili la “Infinix na Tecno ipi ni bora?” Lilitufikia Mtaawasaba na tukafikiri kwa nini tusiandike kuhusu hilo.
Wakati wa kulinganisha bidhaa ni nini kinacholinganishwa Zaidi? Kwanza ni Muundo wa Simu, 2. Ubunifu wa bidhaa na 3. Ubora na Bei ya bidhaa sokoni, Hebu Basi Tuanze;

Cx purple

Ubunifu na Muonekano

Katika siku za karibuni nilitembea katika moja ya maduka yaliyopo Kariakoo kwenye Jengo la China Plaza. Nakumbukuka nilienda kununua simu aina ya Samsung Galaxy S7 edge lakini kwa mara ya kwanza niliona jinala Infinix kwenye simu zilizokuwepo kwenye kabati la kuhifadhia simu. Simu ilikuwa ndogo, nyeusi na imesimama kati ya wengine. Niliitazama ikabidi nimuombe mwenye duka anipatie niweze kuishika mikononi niiangalie vizuri.
Ilikuwa simu nyepesi, skrini ilikuwa laini na yenye kuonekana ni imara. Body ya plastiki kwa nyuma na muundo kama wa chuma kwenye upande mdogo, Camera nzuri, nyembaba na processor ya MTK ram ya kutosha,kwa haraka ilikuwa ni simu nzuri kulingalisha na zile za Tecno.
Kwa sasa simu za Tecno zinashuka kiwango kuuzwa sana hasa kwa kupatikana kwa simu bandia za Tecno hasa katika masoko ya kariakoo, Infinix yenyewe bado imeweza kudhibiti simu zao kwenye simu bandia, Hapa tunaweza kuona Infinix Imeshinda.

Infinix s2 pro vs tecno camon cx
Infinix s2 pro vs tecno camon cx

Ubora na Bei za Bidhaa
Linapokuja suala la ubora wa bidhaa tutalinganisha kati ya Infinix na Tecno kulingana na simu ambazo nimetumia kutoka kwa kampuni hizi mbili: Tecno Camon CX kutoka Tecno na Infinix S2 Pro.
Simu za Infinix na Tecno zinaendeshwa kwenye Android na leo ziko kwenye Android 7.0 Nougat. Kwa suala hili, ufanisi wao ungekuwa sawa. Nini hutofautiana kati ya simu mbili ni kwamba Infinix inatumia interface ya XUI katika Android yake ambapo Tecno yenyewe inatumia Interface ya wa HiOS.
Katika utunzaji wa Charg naweza kusema Tecno ni mshindi hasa katika simu hizi mbili nilizozitumia nilijaribu kutoka na simu moja moja kwasiku tofauti Camon CX ikiwa na asimia mia moja na nikiwa natumia Mtandao wa data siku nzima na games nilirudi nyumbani nikiwa na asilimia 12 lakini Siku ya pili yake nilivyotoka na Infinix haikuweza kufikisha siku nzima kwa matumizi yale niliyoyafanya kama ya kwenye Tecno Camon CX.

Faida za Infinix kwa watumiaji ni kwamba inatoa specification kubwa Zaidi kwa kiwango kidogo cha pesa. Fikiria Infinix S2 Pro 4G, ina betri yenye 3000mAh, skrini ya 5.2 inches, RAM ya3GB) na kuuza kwa TSHs 400,000 tu ikilinganishwa na Tecno Camon CX ilyozinduliwa hivi karibuni.
Simu zote za Tecno na Infix zinatumia Processor zakutoka kampuni ya Mediateck iliyopo China MT65XXX, Screen zinazokaribia kuwa sawa lakini Tecno ni simu popularity Zaidi hapa Tanzania kushinda za infinix na Camera za simu zote hizi mbili hazikuonekana kuwa natofauti katika upigaji na kuchukua video.

Tecno camon cx vs infinix hot s2
Hapa – napenda kusema Tecno inapata mafakio kirahisi kwa sababu watu wengi wanatumia smartphones za Tecno na zimezoeleka.
Tafadhali na wewe tupia comment yako hapo chini na tupige kura  ipi itashinda kati ya Kampuni ya Tecno na infix.

Tufuate @MtaawaSaba ili usipitwe na Habari, Uchambuzi naMakala mbali mbali ya mitanadoni na ya kiteknolojia kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Google+ na Youtube, Pia usisite kutoa maoni yako hapo chini au tuandikie barua pepe kwa mhariri@mtaawasaba.com

Avatar of diana benedict
Mwandishi Diana Benedict Mwandishi
Mitandao ya Kijamii
Diana Benedict. Digital Creator | IT Specialist | Graphics Designer | Web Designer | Web SEO | Contents Management | UI/UX Designer and Social Media Management.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive