Vita ya simu zinazokunjika: Hii ndiyo Huawei Mate X

Maonesho ya vifaa vya elektroniki yanayofanyika kila mwaka huko Barcelona Hispania yameanza na kampuni ya vifaa vya elektroniki kutoka China imekuwa ya kwanza kuonesha vifaa vyao kwa mwaka huu. Siku chache mbele ya kampuni ya Samsung ambao walifanya uzinduzi wao huko Marekani. Huawei wazindua Huawei Mate X. Imepewa jina Simu inayojikunja yenye kasi kubwa zaidi duniani yenye teknolojia ya 5G.

matex

Muundo

Simu ya Huawei Mate X ina muonekano mzuri wa kuvutia kukuteka pale utakapoiona kwa mara kwanza. simu hii tofauti na Galaxy Fold, ina kioo kimoja chenye wembamba wa milimita 5.4 kinapokunjuliwa, na kina milimita 11 kinapokunjwa.

Wakati Samsung wao simu yao inajikunja kwa ndani kama daftari, huawei simu yao inajikunja kwa nje, mtindo walioupa jina la back-to-back fold. hii imewezeshwa na muundo kama bawa la tai.

Safari hii Huawei walijipanga kisawasawa kuleta kifaa kilichoifunika simu ya Samsung, na hata kuilinganisha nayo wakati huohuo kwenye tukio lauzinduzi.

147222-phones-feature-huawei-mate-x-collection-image1-rw82dzshka

Sifa za Huawei Mate X

Huawei Mate X inakuja na prosesa ya Kirin 980 inayotengenezwa na Huawei wenyewe, ikiwa imewekewa modem zenye uwezo wa 5G. modemu hii ina uwezo wa kudownload kwa kasi ya 4.6Gbps. Simu hii inakuja na RAM ya GB 8 na hifadhi ya GB 512. Pia ina uwezo wa kuchomeka line mbili.

Hakuna taarifa nyingi kuhusu kamera ya simu hii japokuwa inajulikana Huawei wana uhusiano na Leica ambao huwatengenezea kamera zao kwa kipindi kirefu sasa. Simu hii ina kamera nne kwa pembeni.

Samsung-Galaxy-Fold-vs-Huawei-Mate-X-the-Big-Battle-of-Foldable-Phones

Simu hii inakuja na betri mbili zenye ujazo wa 4,500mAh, zimepangwa katika mtindo sawa na ule wa Samsung Fold, simu hii inakuja na super chaja yenye watt 55 kwa ajili ya kuchaji kwa haraka. Huawei wanadai inachukua dakika 30 tu kuchaji simu hii kutoka asilimia 0 mpaka 85.

WAWEZA SOMA:  Raia Uganda kutozwa kodi kila watakapotumia mitandao ya kijamii

Bei na upatikanaji

147222-phones-feature-huawei-mate-x-collection-image1-nt1sdxtllk

Simu hii kama ilivo Galaxy Fold, inakuja na bei iliyosimama na ukihitaji inabidi ujipange kisawasawa, maana bei yake inaanzia euro 2299 sawa na shilingi za kitanzania 5,980,000 na itaanza kupatikana madukani kuanzia mwezi Juni 2019. Bei hiii ni ghali kuliko Galaxy Fold.

 

 

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa