Vitu vya kuzingatia unapotaka kununua kompyuta

Mwandishi Alexander Nkwabi

Kununua kompyuta iwe laptop au desktop huwachanganya watu wengi hasa wasiokuwa na uzoefu wa vifaa hivi maana ukifika dukani utakuta za kila namna na miundo tofauti, nimeona niandike makala hii kuwasaidia wale wanunuaji wapya wapate muongozo ili angalau wanapokwenda dukani wajue wanataka nini.

Matumizi

Unapotaka kununua kompyuta, jambo la kwanza ni kujua unataka kwa ajili ya matumizi yapi? kuna watumiaji ambao wao ni kufungua facebook, kusoma barua pepe tu na kutype kazi zake ndogo ndogo hawa wanahitaji pc zisizo na specification kuubwa, kuna ambao wanafanya photoshoping, video editing hawa wanahitaji mashine zenye option kubwa za multimedia.

Bei

Hapa ndo uwa patamu maana, utakuta mtu anataka kompyuta yenye specification kuubwa mfano ram Gb 6, au processor quad core, hard disk %00 GB kuendelea halafu anakwambia ana laki sita, kama huna hela ya kutosha sio tatizo, unaeza ku upgrade kidogo kidogo baadae ukipata hela, mfano nunua ram gb1 then baadae utaongeza mpaka zifike hata 6 kama mashine inaruhusu, au hard disk kama ni ndogo unaweza nunua kisha siku za baadae ukaongeza.​

Mfumo Endeshi

Angalia minimum requirement ya hiyo kompyuta unayonunua, mara nyingi uwa imeoneshwa kuwa hiyo pc imedesgniwa kwa ajili ya operating system gani, zipo kwa ajili ya ubuntu, zipo windows xp, 7, 8 etc

Ukubwa wa umbo

Baadhi ya watu kama mimi napenda skrini kubwa kama desktop haina kuanzia inch 22 au laptop ianzie inc 15 uwa sina raha maana mimi ni mpenzi wa movies na games, jambo la muhimu ni kuwa skirini kubwa ni nzuri kwa wale wenye macho yenye udhaifu. ila kuna ambao wanapenda vile vidogo vidogo labda kwa sababu ni rahisi kubeba nakadhalika.

Matundu

Kutokana na mahitaji yako, angalia kompyuta ambayo itafaa ukiwa umeweka flash pia unaweza kuweka modem, printer nakadhalika, siku hizi kuna hdmi connection, kuna usb 2 na usb 3 ports, matundu ya internet connection​

Jina

Baadhi ya watu kwa sababu moja au nyingine atakwambia amnapenda HP au Dell au Samsung au Toshiba, mfano unaponunua pc ya Hp au samsung unapewa warant ikizingia unaweza irudisha ukatengenezewa au ukapewa mpya,

Hard Disk

kwa watumiaji wa kawaida sio tatiuzo sana hii, ila kwa watumiaji wakubwa{wale wanopenda kudownload softwares mfano adobe suit uwa zina mpaka 5GB} wale wapenzi wa kudownload movies, gaming , na wengineo wanahitaji hard disk kubwa. Magwiji wa komyuta huulizia SATA au SCSI drives

RAM/Memory

Kwa watumiaji wadogo sio ishu sana hii, hata ram ya 2Gb ni kubwa kutosha matumizi ytake yoote. Ila watumiaji wakubwa hasa wale professionals wangependa kutumia kuanzia 4 – 6 GB. pia operating systems kama windows 32bit na 64bit zina minimum requirements za Ram itakayotumika kuziendesha.wataalam wa komyuta wenyewe wakati wa manunuzi huulizia DDR2 au DDR3

Prosesa

Kuna tofauti kubwa sana kati ya processor za single core kama pentium processors, duo-core, na quad core processors,
Kwa mtumiaji wa kawaida PC yenye processor za intel i3 inamtosha saaana
watumiaji wa kati i5 itafaaa ila kwa wale maguru i7 ndio ya kwao​

Waranti

Kama utanunua kifaa chako kutoka katika maduka au mawakala wa hicho kifaa wanaofahamika utapata waranti ambayo itasaidia wewe mtumiaji kupata msaada kifaa kitakapopata matatizo mfano battery ikizingua kama hujaiharibu mwenyewe unaweza kubadilishiwa ukapewa ingine na kadhalika.

Kwa leo tuishie hapa, kama umepata chochote hapa, Gonga Like, maswali, michango mingine yoyote inakaribishwa

Avatar of alexander nkwabi
Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive