Vodacom Tanzania imezindua huduma ya teknolojia ya 5G

Mwandishi Alice

Kwa mara ya kwanza kabisa Watanzania wataanza kutumia teknolojia ya mawasiliano ya 5G kwani kampuni ya Vodacom Tanzania imezindua huduma ya teknolojia 5G ikisema italeta mapinduzi na kuongeza ushiriki wa Taifa katika kuleta mageuzi ya nne ya viwanda. Hii inafanya Tanzania kuwa moja ya nchi za mwanzo kabisa barani Afrika kutumia huduma ya teknolojia yenye kasi ya 5G

Teknolojia hii ya 5G inakuja na fursa kubwa hapa nchini kwa wabunifu kuleta bidhaa na huduma mpya kwa wananchi. Vodacom sio tu itaendelea kubuni huduma mpya bali kuwezesha jamii ili kutimiza ndoto za kujenga Taifa bora.’ Hayo yameelezwa leo Alhamisi Septemba Mosi, 2022 na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Hilda Bujiku

Katika uzinduzi huo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye aliyeeleza kuwa, Mei mwaka huu aliahidi Bungeni kwamba Tanzania itaanzisha 5G hapa nchini jambo hilo limetia leo kwa kampuni ya Vodacom kulitekeleza.

“Tuliposema ilikuwa kama ndoto lakini leo karibu miezi mitatu, lakini Vodacom wametekeleza na kutusaidia kuingia kwenye orodha ya nchi chache Afrika zilizoanzisha huduma ya teknolojia ya 5G.Vodacom wamekuwa wa kwanza kwenye mambo mengi wameanza na M-Pesa na mambo mengine nawashukuru,” amesema Nape.

Mpaka sasa nchi za barani Afrika ambazo zimeanza kutumia teknolojia hii ya kasi ya 5G ni pamoja na  Kenya, Misri, Afrika Kusini, Uganda na nyinginezo.

Akitoa ufafanuzi zaidi, Mkurugenzi wa Huduma za Mtandao wa Vodacom, bwana Andrew Lupembe, amesema huduma hiyo inatarajiwa kuanza kupatikana katika baadhi ya mikoa kama Dar es Salaam, Njombe, Dodoma, Arusha, Mwanza na mingine kuanzia Novemba 2022. Ambapo kwa sasa huduma hiyo itaanza kupatikana kwa wateja ambao ni kampuni na vifaa vya intaneti kama Routers.

 

Mwandishi Alice Mhariri Mkuu
Mitandao ya Kijamii
Alice ni mwandishi na mhariri wa makala mbalimbali hapa Mtaawasaba tangu mwaka 2016. Akiwa hayupo kazini hupendelea kusoma vitabu, kuogelea na kusikiliza muziki
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive