Vodacom Yaanza Majaribio Matumizi ya 4G

Alexander Nkwabi Maoni 154
Vodacom Yaanza Majaribio Matumizi ya 4G. Wateja wa Vodacom sasa wanauwezo wa kutumia teknolojia ya Long Term Evolution – LTE ambayo ni ya kisasa zaidi ulimwenguni katika utoaji wa huduma za Mawasiliano na hivyo kupunguza gharama katika kuwasiliana kufuatia kampuni hiyo kwa kushirikiana na Kampuni ya Nokia Siemens kuwawezesha wateja wake kufanya hivyo katika mradi wa majaribio unaohusisha eneo la Msasani jijini Dar es salaam.

Majaribio hayo yanafanywa kwa ushirikiano na kampuni ya Nokia Siemens yatahusisha eneo lote la Msasani jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwawezesha wateja wa kampuni hiyo kuona ubora wa teknolojia hiyo katika kupokea huduma za simu za mkononi ikiwemo kupiga simu, kutumia huduma za Intaneti n.k

003.LTE

Ni hatua nyingine muhimu kutoka Vodacom tunapowawezesha wateja wetu kupata kile ambacho ni wazi kitawapunguzia gharama katika matumizi ya huduma zetu sokoni bila ya kuwepo na mabadiliko ya gharama. “Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza wakati akitangaza rasmi kuanza kwa majaribio hayo leo jijini Dar es salaam LTE inayofahamika pia kwa jina la 4G ndio teknolojia ya kisasa zaidi ulimwenguni ambayo imedhihirisha uwezo wa hali ya juu katika mawasiliano ikiwemo huduma za intanteti katika kudadavua mitandao kupata filamu, machapisho, michezo ya kwenye kompyuta n.k

Kwetu sisi kuwawezesha wateja wetu kuweza kuijaribu teknolojia bora na ya kisasa zaidi ni kielelezo cha namna ambavyo Vodacom inavyoishi kimatendo kwa dira yake katika kuongoza mageuzi katika sekta ya huduma za simu za mkononi nchini.

Alisema Meza na kuongeza kuwa “Tunaona fahari kubwa namna kampuni yetu inavyokwenda sanjari na wimbi la mabadiliko ya teknolojia lililopo katika muktadha wa utandawazi, na namna inavyozitumia kwa ufasaha faida za kiteknolojia siku hadi siku katika kukidhi matakwa ya wateja wake.

008.LTE

Meza amesema Vodacom imeanza na Msasani kutokana na eneo hilo kuwa na uwiano mzuri wa shughuli za kibiashara na makazi ambazo zote zinahitaji huduma za Intaneti zenye kasi za kiwango cha LTE ingawa mipango ni kuisambaza teknolojia hiyo katika maeno mengine nchini “

Tunatambua kuwa njia za masafa ya hewa ya mawasiliano kwa mfumo wa LTE kwa sasa zimejaa hapa nchini hata hivyo bado Tanzania haijafikiwa kwa ukamilifu na huduma za Intaneti zenye kasi, hivyo basi ni matumaini yetu kwamba serikali itatupatia muongozo ili nasi kupitia mtandao mpana wa Vodacom tuwwawezeshe watanzania wengi zaidi kufikiwa na huduma za Teknohama zenye ubora unaoendana na mahiraji ya sasa.”

007.LTE

Kwa upande wake, Mkuu wa huduma za Vodacom katika kampuni ya Nokia Siemens Pete Beadle, alisema kiwango cha juu cha teknolojia za mawasiliano ndani ya kampuni hiyo duniani kote imekuwa ni chaguo la majaribio kwa kampuni zinazotoa huduma zinazozingatia teknolojia za kisasa, kutokana na dhana yake ya mwingiliano wa zaidi ya teknolojia moja na kwa lengo moja linalozingatia matakwa, kasi na viwango vya ubora.

Beadle, aliongeza kuwa kiuhalisia na kwa kuzingatia mahitaji ya soko nchini, Vodacom ndio kampuni pekee iliyojipanga kutoa huduma hiyo ya kasi kwa kuwa tayari. Hadi sasa imekwisha kamilisha awamu ya kwanza ya upitishaji wa huduma zake katika mkongo wa taifa wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (NICTBB) pamoja na ule wa mawasiliano wa baharini unaopita sehemu kubwa duniani.

@Mtaawasaba

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive