Baada ya kuachwa nyuma na App zingine zinazotoa huduma ya kutuma na kupokea jumbe kama Telegram, hatimaye WhatsApp yazindua Community Chats, Emoji Reaction, na zana kwa ma Admin.
WhatsApp kwa muda sasa wamekuwa wakifanyia kazi vipengele vya Reactions na Community, na sasa wametangaza rasmi kuzindua vipengele hivyo. Haya ndiyo unayotakiwa kuyafahamu.
Kupitia press release waliyoandika, kipengele cha Communities kitakuwa ni mahususi kwa taasisi lama shule na klabu ndogo ndogo, bila kusahau taasisi zinazojitolea.
Maboresho pia yataonekana kwenye makundi ambapo sasa itawezekana hadi watu 32 kuongea kwenye audio call kwa wakati mmoja, reactions, uwezo wa kutuma mafaili makubwa ya mpaka gb 2, na pia sasa admin wa kikundi ataweza kufuta ujumbe wowote.
Reactions – Emoji Reaction ni kipengele kinachomuwezesha mtumiaji ku react kwenye ujumbe husika moja kwa moja bila kuweka emoji zinazojitegemea
Admin Delete – Sasa wasimamizi wa makundi wataweza kufuta ujumbe wowote kutoka mtu yoyote.
File Sharing – Sasa itawezekana kutuma ma faili yenye ukubwa wa mpaka 2GB.
Larger Voice Calls – Sasa itawezekana watu hadi 32 kuongea kwa pamoja kwenye audio call.
Mkurugenzi mtendaji wa WhatsApp, bwana Will Cathcart, ametangaza kuwa Reaction kwa sasa zitakuwa na emoji sita tu, ila kadri siku zinavyoendelea zitaongezwa emoji zaidi na muonekano kama instagram.
Mtaawasaba itakujuza mpenzi msomaji wetu vipengele hivi vitakapoanza kuonekana. Unazungumziaje maboresho haya? Tuandikie kwenye comment hapo chini, pia usisahau kutuandikia kwenye mitandao ya kijamii