Wireless Storage: Njia rahisi ya kuhamisha Data kwenye simu yako ya android.

Data transfer imekuwa kikwazo kikubwa hasa katika file kubwa mfano file yenye kuanzia 1gb na zaidi inakuwa inachukua muda mrefu sana kutumia USB cable au kwa njia ya Bluetooth ndio itachukua muda mrefu zaidi.

Nakuletea kwako wireless data transfer ambayo itaweza kuifanya simu yako kuwa kama server ndogo na kuweza kuuunganisha na watu zaidi ya watano ambao wote wataweza kuongeza files na kupakua files kutoka kwenye simu yako. Njia hii ni rahisi na naweza kusema ni Namba moja duniani kuliko kutumia USB cable au Bluetooth. Acha kupoteza muda wako au kupata usumbufu wa kuchomoka kwa usb cable kila unapokopi data kwenye computer yako au simu nyingine ya android.

Pia tukiacha andoid tu zipo hard driver nyingi zimezinduliwa miaka iliyopita kufanya kazi hiyo ambayo inafanya kazi kama program hii.

Wireless Transfer ni nini?

Wireless Transfer (FTP) Ni njia rahisi na salama ya kuhamisha au kugawanyisha file kwa haraka zaidi bila kutumia kiunganishi chochote cha waya. Njia hii hutumia wireless Connection yaani Wi-Fi.

Inafanyaje kazi?

Wireless transfer inafanya kazi kwa kuweka aina mojawapo ya programu zinazopatikana play store au hata kwa kuna njia nyingine ambayo unaweza ifanya kwenye simu yako laini rahisi zaidi nii ninayokuletea ambayo unainstall app kwenye simu yako ya android na kutengeneza kitu kama server ambayo itakupa wewe mtumiaji link maalumu ambayo utaiweka kwenye computer yako upande wa files na kukupa username na password ambayo utaijaza na kuweza kupata files zote zilizopo kwenye simu yako. mpaka hapo utakuwa na uwezo wa kuongeza files kutoka kwenye computer yako na kuweka kwenye simu au kuhamisha files zilizopo ndani ya simu na kuziweka kwenye computer.

WAWEZA SOMA:  Google yanunua sehemu ya HTC kwa dola bilioni 1.1

 

Njia za kufanya.

  1. Download Wi-Fi Transfer kwenye simu yako ya androidunayotaka kukopi files. nitaweka download link hapo chini, vile vile unaweza tafuta bora zaidi kwenye play store ila narecomend kudownload hii.
  2. Ukishadowanload ifungue na itakupa link maalum ambayo utaitumia kwenye simu yako au pc nyingine na unaweza mpa mtu yeyote ambae yuko karibu yako.
  3. Set up Mobile hotspot na uwashe mobile hostpot na uunganishe kwenye device unayohitaji unaweza unganisha zaid ya device 10 inategemea na speed ya proccesor yako.
  4. Sasa utaweza kustart ftp server na utapata link ambayo iko kama hivi ftp://192.168.43.1:888 (inategemea na device) huna haja ya internet connection labda tu ikiwa hujadownload bado programu hiyo.
  5. Utaweka link hiyo kwenye browser yoyote hata chrome lakini kwa watumiaji wa windows ingependeza zaidi ukaweka upande wa my computer na kama unatumia android download es file exproler nauende upande wa network > ftp na utaweka link hiyo.

EF File Exproler

Wifi Storage Download Playstore

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa