Nini cha kutarajia katika mkutano wa WWDC 2018

Apple wako tayari kwa ajili ya mkutano wa mwaka 2018 wa ma developer duniani kote maarufu kama Worldwide Developers Conference (WWDC) utakaofanyika Jose McEneryxf Convention Center maeneo ya San Jose, California. Tukio hili litadumu kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 4 mpaka 8 ya mwezi wa sita 2018.

Kama jina la mkutano linavosema, tukio hili la WWDC linahusu zaidi ma developer, japo kuna vitu kadhaa ambavyo vitagusiwa kwa upande wa watumiaji kwenye keynote. Inasemekana mkutano wa mwaka huu utajikita zaidi kwenye upande wa software kuliko hardware.

Sio rahisi kujua Apple wameandaa nini kwa ajili yetu, kwa mujibu wa tetesi mbalimbali mitandaoni baadhi ya mambo tunayatarajia kuyaona kwenye mkutano huu mkubwa unaofanyika mara moja tu kwa mwaka ni pamoja na mifumo mipya na iliyoboreshwa ya software, ambayo ni pamoja na macOS 10.14, iOS 12, watchOS 5 na tvOS 12.

Usikose Kusoma:  Vitu 6 vilivyogunduliwa na wanawake na kubadili dunia

iOS 12

Majuma kadhaa yaliyopita Apple waliachia maboresho ya mfumo endeshi wake kwenye toleo la iOS 11.4. Katika toleo hili mapoja na marekebisho kadhaa, waliongeza uwezo wa ufanyaji kazi kwenye kifaa cha HomePod.

Matarajio makubwa kuhusu mfumo endeshi huu ni toleo la iOS. Tetesi zinadai kwamba iOS 12 litakuwa ni toleo kubwa litakalokuja na maboresho mengi ikiwa pamoja na vitu kadhaa vitakavyoongezwa kutoka mfumo endeshi tangulizi.

Maboresho ya mfuno wa NFC

Moja ya vitu vinavyosemwa sana ni maboresho makubwa ya NFC (Near Field Communication) ambapo sasa kupitia toleo hili jipya utaweza kutumia simu yako kufungua milango ya gari, nyumba, pia itaweza kutumika kulipia kwenye njia za usafiri kama tunavyofanya (wale wenye kadi) kwenye mwendokasi, au pantoni.

Digital Health

Kunatarajiwa kuongezwa feature ya ‘Digital Health’ ambayo itamsaidia mtumiaji kujua anatumia muda kiasi gani kwenye kifaa chake na pia kwa app moja moja. Pia itakuwezesha kujua ume unlock simu yako mara ngapi kwa siku.

Usikose Kusoma:  Sasa kupitia WhatsApp unaweza kupiga simu za sauti na video kwa hadi watu wanne

Animoji kwenye FaceTime

iOS-11.3-Animoji

Ripoti kadhaa zinaonesha kutakuwa mpango wa kuongeza Animoji kadhaa kwenye simu ya iPhone X. Na haikuishia hapo tu, inasemekana Animoji zitaanza kupatikana kwenye Facetime, japo haijulikani kama hili litatangazwa kwenye tukio hili au watatangazawakati mwingine.

Mengine

vitu vingine vinavotarajiwa kuwepo ni pamoja wa uzinduzi wa ARKit 2.0 ambayo itakuja na iSO 12, hii ikiwa ni maboresho ya mtangulizi wake ARKit 1.5 SDK. Mengineyo ni maboresho makubwa kwa mfumo endeshi ikiwemo kurekebisha makosa mbalimbali, na kuongeza maboresho.

Endelea kuwa nasi kila siku tukikuangazia kila kitakachokuwa kinajiri kwenye mkutano huu mkubwa wa Apple. Usisahau kusbscribe kwenye channel yetu ya YouTube, Tufuate Instagram, twitter na facebook ili uwe kwanza kupata taarifa mbalimbali za teknolojia.

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa