YouTube kuongeza njia zaidi kujiingizia kipato kwa watengeneza maudhui ikiwemo kupokea fedha moja kwa moja kutoka kwa watazamaji na pia kupitia kuuza na kununua bidhaa.
Hayo yametajwa kupitia chapisho refu kwenye blogu ya YouTube ambapo inatarajiwa kuzindua Youtube Shorts (mfumo wa video zilizosimama kama TikTok) kwa watumiaji wa Marekani, kwa sasa kipengele hiki kilizinduliwa nchini India.
Kipengele cha YouTube Shorts kitaongezewa uwezo zaidi ili kurahisisha uchapishaji wa maudhui, baadhi ya mambo yatakayoongezwa kwenye shorts ni pamoja na uwezo kuweka video effects na uwezo wa ku hariri video kabla haijachapishwa, pia uwezo wa kujibu maoni ya watazamaji moja kwa moja kwenye video kama ambavyo inawezekana kwenye TikTok.
Pia, ili kuongeza njia zaidi za kuongeza kipato kwa wachapisha maudhui, YouTube ina mpango wa kuanzisha uwezo wa kuingiza pesa kupitia Shorts kwa kuleta vipengele kama branded content, super chat, uwezo wa kuruhusu kuuza bidhaa moja kwa moja kupitia shorts.
Kwenye chapisho hilo imeandikwa, Uwezo wa kufanya manunuzi utasambazwa kwenye karibia kila kipengele kilichopo YouTube ili kumnufaisha mtengeneza maudhui huku wakiendelea kuangalia namna bora zaidi ya kuunganisha huduma ya manunuzi na Utumiaji wa mtandao wa kijamii wa YouTube