YouTube yazindua mfumo mpya wa utafutaji ili kurahisisha upatikanaji wa video

Mwandishi Alexander Nkwabi

Ili kuwezesha watumiaji kugundua vile wanavotafuta kwenye Youtube ambayo inamilikiwa na Google, wamezindua maboresho katika upande wa utafutaji wa video mbalimbali kwenye tovuti hiyo. Kwa maboresho haya, sasa utaweza kuona sura (chapter) moja kwenye matokeo ya utafutaji, pia utaweza kuona preview ya video moja kwa moja kwenye app ya simu za mkononi, na mwisho utaweza kuona matokeo yenye lugha tofauti yakiwa yametafsiriwa moja kwa moja.

Maboresho kwenye utafutaji

1. upatikanaji wa sura (chapters) kwenye matokeo ya utafutaji

Maboresho ya kwanza kabisa ni kuongeza upatikanaji wa sura (chapters) kwenye matokeo ya utafutaji ukiwa Youtube. Hii ni muendelezo wa uboreshaji ya mfumo wa video zenye chapters ambao ulizinduliwa mwaka jana. Mfumo huu humuwezesha mtengeneza video kuchapisha video ambayo inaweza kugawanywa katika vipande vipande (sura mbalimbali) na hii inamrahisishia mtazamaji kwenda moja kwa moja kwenye kipande anachotaka kukiona badala ya kuangalia video nzima kama ilivyokuwa hapo awali.

youtube chapters 1

2. uwezo wa ku preview video kwenye ukurasa wa matokeo kwa simu za mkononi

maboresho ya pili ni uwezo wa kuona kinachoendelea kwenye video husika hata kabla ya kuifungua, kabla ya hapa waliokuwa wanaweza kupata huduma hii ni watumiaji wa YouTube desktop tu ila kwa sasa watumiaji wa simu za mkononi wataweza pia, ambapo pale unaposegeza kasa kwenye video itaanza kucheza hata kabla hujaifungua, hii itasaidia watumiaji kutofungua video ambazo sizo wanazotaka.

3. Tafsiri kwenda lugha zingine kwenye video

Mwisho, inawezekana umetafuta video ila unayotaka kuiangalia haiko katika lugha unayoijua, basi sasa hivi unapotafuta video kwenye simu ya mkononi YouTube watakuletea video zenye lugha tofauti na unayotumia zikiwa zimetafsiriwa kwa maandishi moja kwa moa, hii itahusisha jina, maelezo ya video pamoja kitakachokuwa kinazungumzwa kwenye video. hii itasaidia watumiaji kuongeza wigo wa utazamaji wa video mbalimbali

YouTube new search features 3

pamoja na maboresho haya ya YouTube kwa watumiaji wa desktop na simu za mkononi dunia nzima, pia YouTube wanafanyia majaribio huduma mpya zinazohusisha upatikanaji wa video kwenye mtandao wa utafutaji wa Google Search.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive