Zimbabwe kutumia teknolojia ya alama za vidole kwenye uchaguzi wa 2018

Serikali ya Zimbabwe imetangaza kuwa imeingia mkataba wa kusambaza vifaa na teknolojia ya kutambua alama za vidole kwa kampuni ya kimarekani Ipsidy.  Kmapuni hiyo inatarajiwa kusambaza vifaa pamoja na software vitakavyozuia mtumiaji kupiga kura zaidi ya mara moja kwa kutumia alama za vidole. Watajumuisha Automated Fingerprint Identification System (“AFIS”) mfumo ambao utatumika kwenye uchaguzi unatarajiwa kufanyika baadaye mwaka 2018.

Kampuni ya Ipsidy ilichaguliwa baada ya kushinda tenda ya kusambaza vifaa vya kupigia kura na teknolojia husika. Mkataba huo ulisainiwa na kamisheni ya uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC)

Ipsidy inasema itaunganisha daftari la wapiga kura na teknolojia yao ya AFIS, ambapo itapatikana orodha na idadi kamili ya wanaostahili kupiga kura kwenye uchaguzi huu unaotarajiw akufanyika siku zijazo mwaka huu. Database ya wapiga kura ya zimbabwe ilianzishwa mwaka 2017 na imekuwa ikitumika kujua watakaostahili kupiga kura kwenye chaguzi mbalimbali.

Tangazo la kuchaguliwa Ipsidy. linakuja miezi michache baada Raisi Robert G. Mugabe kuvua madaraka yake kama raisi wa nchi ya Zimbabwe ambae amehudumu kwa miongo kadhaa akiwa kwenye nafasi hiyo. Mugabe alikuwa akituhumiwa kuchakachua matokeo ya uchaguzi kila mara.

Ipsidy ina makao makuu yake jijini New York Marekani na imefungua matawi kadhaa nchini Colombia na Afrika ya kusini.

WAWEZA SOMA:  Kashfa ya Cambridge Analytica yafanya Facebook kuzindua programu kusafisha mipangilio yako ya faragha.

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa