Uchambuzi wa Windows 11: Je unahitaji ku upgrade kutoka Windows 10?

Alice 1 161
Zimepita siku kadhaa tangu Microsoft kuachia mfumo endeshi wa Windows 11. Toleo hili ni moja ya matoleo makubwa ya mfumo endeshi huu wa kompyuta kuachiwa ikiwa ni sasisho la bure kwa watumiaji wa toleo lililotangulia la Windows 10. Huu ni uchambuzi wa Windows 11.

Mtaawasaba imepata nafasi ya kutumia Windows 11 ambayo imekuja na muonekano mpya na wa kitofauti kidogo na watangulizi wake, na tumekuja na uchambuzi ambao utagusia hili la muonekano na mengine, bila kusahau swali la muhimu kabisa la, Je ni sawa ku update kwenda toleo hili jipya kwa sasa au ni bora kusubiri?

Untitled12345678

Mahitaji ya chini (minimum requirements)

Kabla ya kuanza kuchambua, tufahamu kwanza mahitaji ya chini kabisa. ili kompyuta iweze kupata sasisho la Windows 11 ni lazima iwe na;

  • Prosesa lazima iwe na 1 GHz au zaidi na iwe angalau ni  dual-core 64-bit kutoka IntelAMD, au Qualcomm.
  • RAM kuanzia 4GB na kuendelea.
  • nafasi ya uhifadhi kuanzia 64GB.
  • iwe na UEFI Secure Boot inayokubalika na isiwe imezimwa.
  • Pia iwe na Trusted Platform Module (TPM), toleo 2.0.
  •  GPU yenye kukubali Direct X 12
  • kioo chenye ukubwa kuanzia inchi 9 na chenye kuonesha kuanzia 720p.
  • na mahitaji mengine mengi unaweza yasoma hapa

Muonekano mpya

kitu cha kwanza unachokutana nacho pindi unapofanikiwa kusanikisha mfumo endeshi huu ni muonekano mpya, ambapo utakutana na;

  • start button ambayo iko katikati ya task bar, japo kuwa inaweza kubadilishwa kupitia settings kurudi upande wa kushoto wa taskbar kama ambavyo tumezoea kwenye matoleo yaliyopita
  • start menu tofauti na ile tuliyoizoea, unabofya kitufe cha windows unakutana na start menu tofauti kidogo inayovutia
  • icon mpya, wallpaper na theme mpya ambazo zinakuja na light na dark mode.
  • kona zilizojikunja, tofauti na matoleo yaliyopita, toleo hili linaonekana kunakili au kufanana kimuonekano na mac os na chrome os kwa namna moja au ingine,
  • milio, imekuja na milio mipya ambayo haikeri,

windows 11

Mabadiliko mengine ambayo utayaona ni kurudishwa kwa widget ambazo mwanzo tuliziona kwenye windows 7 na zikaondolewa kwenye matoleo yaliyofuata. Pia windows store imebadilshwa na kuwa Microsoft Store ambayo imepata muonekano mpya pia, ambayo inasemekena itakuwa na uwezo kufungua app za android japo kwa sasa haijawa rasmi.

Untitled1234

Urahisi wa kutumia

Windows 11 ni nyepesi kama ambavyo unatumia Windows 10, na programu zote ambazo zinakubali kusasishwa kwenye Windows 10 pia zinakubali kwenye toleo hili na zinafanya kazi bila kukwama.

Je unahitaji ku upgrade kutoka Windows 10?

Kutokana na mahitaji ya chini kabisa ya kupata sasisho la moja kwa moja la Windows 11, kompyuta nyingi ambazo zimetengenezwa miaka kuanzia minne iliyopita na kurudi nyuma hazitaweza kupata, hata hivyo unaweza ku download Windows 11 mwenyewe na ku sasisha kwenye kompyuta yako.

Kwa mtazamo wetu, Windows 11 bado inaendelea kufanyiwa maboresho na tunashauri usubiri angalau miezi kadhaa kabla hujaamua kutumia Windows 11, hii ni kama kompyuta yako ina vigezo vya kupata toleo hili.

Kwa ufupi

Mazuri

  • Muonekano mpya ni wa kuvutia
  • Maboresho kwenye utendaji wa kazi kuliko mtangulizi wake Windows 10
  • Msisitizo wa ulinzi wa kompyuta kwa kusisitiza matumizi ya Secure Boot na TPM.
  •  Maboresho mengine mengi kwenye apps na matumizi ya kalamu kwenye skrini
  • Sasisho la bure kama ulikuwa unatumia Windows 10.

Changamoto

  • Bado kuna baadhi ya mabaki ya matoleo yaliyotangulia, mfumo haujabadilishwa wote.
  • Taskbar imezuiwa kubadilisha (huwezi kuongeza ukubwa wa taskabar au kupunguza)
  • Widgets still feel mostly pointless in their latest iteration.
  • hakukuwa na ulazima wa kurudisha Widget
  • Lazima uwe na internet ili uweze kukamilisha hatua za mwanzo (Windows 11 home)
Mwandishi Alice Mhariri Mkuu
Mitandao ya Kijamii
Alice ni mwandishi na mhariri wa makala mbalimbali hapa Mtaawasaba tangu mwaka 2016. Akiwa hayupo kazini hupendelea kusoma vitabu, kuogelea na kusikiliza muziki
1
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive