Sera Ya Faragha

Makubaliano haya na Sera ya faragha inahusu tovuti, aplikesheni na/au huduma zingine, bila kujali zimesambazwaje, zimechapishwaje au zimetolewa na Mtaawasaba pamoja washirika wake ambao wanahusika na mkataba huu wa makubaliano, ambao unawabana wote wanaopata huduma, mtu binafsi au kwa niaba ya kikundi, ikiwemo wewe, kikundi ama injini za kidijitali zinazoweza kupata, kupekua, kunakili taarifa zetu.

Sisi kama Mtaawasaba tunafurahia utembeleaji wako au utumiaji wako wa huduma zetu ndio maana tumeona umuhimu wa faragha yako. Sera hii ipo kwa ajili ya kukufanya uelewe namna sahihi ya utumiaji wa taarifa ukiwa katika tovuti yetu.

 

Matumizi ya taarifa binafsi

Sio lazima kujiunga ili utumie huduma zetu. Hata hivyo tovuti yetu inaweza kuwa na huduma ya kutoa maoni, uchangiaji wa mada, kupiga kura na kadhalika. Huduma hizi zitakuhitaji kujisajili ili uweze kutumia huduma izo. Kama wakati wa kujisajili ikitokea ikakulazimu kutoa taarifa zako binafsi, hakuna taarifa zako binafsi tutakazo zisambaza kwa mashirika mengine labda kwa ridhaa yako. Kama utaacha maoni au utaandika makala ambayo itaonekana kwa hadhira hatutakuwa na namna ya kuzuia watu wengine kuzitumia taarifa zako binafsi.

Pia tunawaruhusu wasomaji wetu kupata fursa ya kujiunga ili wapate kuwasiliana nasi kwa urahisi. Tunaweza kukuuliza taarifa binafsi. Kutegemeana na anachotaka msomaji, haya mawasiliano yanaweza kuwa kama ifuatavyo; makala ya kwa njia ya barua pepe, taarifa za kampuni yetu, na / au ofa mbalimbali. Unaweza kujitoa kupokea mawasiliano kwa kubofya kitufe cha kujitoa ambacho huambatanishwa kwenye barua pepe tunazotuma, au kwa kutuandikia kwa barua pepe kuhusu kutaka kujitoa kwenye huduma husika.

Kama utatupa taarifa zako binafsi kwa ajili ya kupokea huduma hizo hapo juu basi taarifa zako hazitatumiwa na makampuni mengine labda kwa idhini yako tu. Kama taarifa zako binafsi zitabadilika ama hujisikii tena sisi kuendelea kuwa na taarifa zako, unaweza omba masahihisho, marekebisho ama kufutwa kwa taarifa zako kwa kutuandikia kwenye mhariri[at]mtaawasaba.com

 

Viunga vinavyotoka nje

Tovuti hii inaweza kuwa na viunga vinavyoelekeza kwenda kwenye tovuti zingine ambazo hatuzisimamii. Hatutawajibika kwa sera na faragha za mitandao isiyo na uhusiano na sisi.

 

Kuki na matangazo ya biashara

Tunatumia makampuni mengine kutangaza kwenye tovuti yetu pale unapotembelea. Haya makampuni hayana taarifa zako binafsi (ikiwemo jina lako, anwani au namba ya simu) lakini yatatumia taarifa zisizo za kibinafsi kuhusu tabia yako ya utembeleaji wako wa tovuti ili kuleta matangazo. Kama una maswali zaidi kuhusiana na hili unaweza kutuandikia kwenye anwani tuliyoweka chini kabisa.

 

Usalama

Tunafuata utaratibu unaokubalika kimataifa katika kuhifadhi taarifa binafsi za wasomaji/wateja wetu. Hata hivyo hakuna njia ya kuhifadhi taarifa kielektroniki iliyo salama kwa 100%. Kwahiyo hatuwezi kukuhakikishia usalama wa taarifa zako.

 

Kujitoa kisheria

Tuna wajibu wa kuhifadhi taarifa binafsi za wateja wetu kama tunavyotakiwa na sheria. Pia  tunaamini kuwa ni lazima kuhifadhi taarifa za wasomaji wetu isipokuwa kwa ajili ya shauri la kisheria, amri ya korti ama taarifa zozote za kisheria zitakazoletwa kwenye tovuti yetu.

 

Mawasiliano

Kama una maswali, maoni au kitu chochote kuhusiana na sera hii, basi usisite kutuandikia kupitia [email protected] au ukurasa wetu wa mawasiliano

 

sera ya faragha

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive