Kupitia ripoti iliyochapishwa na mtandao wa The Verge siku ya jumanne, Kampuni ya Facebook mbioni kubadili jina
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Facebook bwana Mark Zuckerberg, anatarajiwa kuzungumzia mabadiliko haya ya jina kwenye mkutano wa mwaka wa Connect conference mnamo tarehe 28 mwezi wa 10, 2021. Hata taarifa hii imetoka mapema kabla ya muda kupitia chanzo cha kuaminika (ambacho hakikutaka kujulikana).
Makampuni makubwa uwa yana tabia ya kutengeneza kampuni kubwa moja inayosimamia makampuni mengine yote, mfano Google walianzisha kampuni ya Alphabet mwaka 2015, na inaonekana kampuni hii mpya ndiyo itakuwa ikisimamia makampuni mengine kama app ya Facebook, Instagram, Whatsapp, Oculus na mengine ambayo yako chini ya kampuni ya Facebook.
Kwanini Facebook Mbioni Kubadili Jina? Wazo la Facebook mpya ni kujikita zaidi kwenye “metaverse” – mazingira yanayoendeshwa na kompyuta ambapo watu wanaweza kuwasiliana kupitia teknolojia kama Artificial Intelligency (uelewa wa kutengenezwa) na Virtual Reality pamoja na teknolojia zingine za namna hiyo. Facebook imekuwa na wazo hili tangu iliponunua kampuni ya vifaa vya kuvaa kichwani vya virtual reality ya Oculus mwaka 2014.
Taarifa hii ya Facebook kutarajia kubadili jina imekuja baada ya tangazo ajira zipatazo 10000 zilizotangazwa na Facebook kwa nafasi zinazohitaji utaalamu huko umoja wa ulaya kupitia kampuni yake ya Horizon Worlds kwa miaka mitano.
Mitandaoni watu wameanza kukisia jina la kampuni hii mpya linaweza kuwa FB, Meta au Horizon. Hata hivyo Facebook wamegoma kuzungumzia ripoti hii wakisisitiza uwa hafanyii kazi tetesi.