Siku kadhaa zilizopita mtandao wa the Verge ulichapisha taarifa ya kwamba Kampuni Ya Facebook Mbioni Kubadili Jina. Taarifa ya Facebook kubadili jina na kuitwa Meta imekuja leo kupitia kwa mkurugenzi mtendaji wa Facebook, Mark Zuckerberg ambapo amesema Facebook inabadili ili kujitofautisha na mtandao wa kijamii wa Facebook kwani kampuni iyo kwa sasa inajihusisha na mambo mengine mengi tofauti zaidi ya mtandao wa kijamii huo.
kampuni yetu inahusishwa kwa karibu na bidhaa moja ambayo haiwakilishi kila kitu tunachofanya kwa sasa, na baadaye – mark Zuckerberg
Akiongea kwenye mkutano wa ndani wa kampuni uitwao Connect, Zuckerberg ametangaza jina jipya la kampuni litakuwa Meta. Na Sasa kupitia utaratibu mpya, Facebook na mkusanyiko wa app na huduma zingine zitakuwa chini ya kampuni kubwa ya Meta, ambayo itakuwa chini ya Zuckerberg.
Taarifa ya Facebook kubadili jina na kuitwa Meta inakuja baada ya kampuni ya Facebook kukosolewa sana kutokana na kuvuja kwa “taarifa za ndani” kuvujishwa na mtumishi wa zamani wa Facebook. Nyaraka hizo zina taarifa zinazoonesha jinsi taarifa za watu mashuhuri kutenganishwa na watu wengine, pia zikionesha jinsi kampuni ilivoshindwa kusimamia na kuzuia vikundi vyenye misimamo mikali kutumia mtandao wa Facebook kwenye uchaguzi wa marekani mwaka 2020, pia utafiti unaoonesha jinsi Facebook inavoahatarisha afya za vijana.
Facebook kubadili jina na kuitwa Meta kutaathiri kampuni tu, na sio mtandao wa kijamii wa Facebook, Instagram, Whatsapp na huduma zingine zote zitasalia na majina yao. Jina hili jipya litasaidia kuonesha uelekeo wa kampuni hii ambao ni “metaverse” – mazingira yanayoendeshwa na kompyuta ambapo watu wanaweza kuwasiliana kupitia teknolojia kama Artificial Intelligency (uelewa wa kutengenezwa) na Virtual Reality pamoja na teknolojia zingine za namna hiyo. Facebook imekuwa na wazo hili tangu iliponunua kampuni ya vifaa vya kuvaa kichwani vya virtual reality ya Oculus mwaka 2014.
Facebook sio kampuni ya kwanza kufanya mabadiliko ya jina kwa namna kama hii, mwaka 2015 Google walibadili mfumo wa kujiendesha na kuanzisha kampuni mama waliyoiita Alphabet. Ambapo Google ikabaki kuwa sehemu ya Alphabet, tofauti na Facebook ambayo inabadili kwa sababu tofauti na kuhakikisha inajitenga na jina la mtandao wake wa kijamii.