Vodacom Tanzania waja na M-Pesa visacard

Alice 2 175
Vodacom Tanzania waja na M-Pesa visacard. Kama wewe ni mmoja kati ya watumiaji wa kadi za manunuzi mtandaoni kupitia mtandao wa Vodacom Tanzania basi utakuwa umepata ujumbe mfupi wa maneno ukikujulisha kuwa kuanzia sasa Vodacom wanasitisha huduma hiyo kwa kutumia kadi za Mastercard.

voda mastercard ujumbe

Pia Vodacom, wametuma ujumbe unaowataka watumiaji ambao walikuwa na akiba ya fedha kwenye kadi zao za awali za mastercard wahamishe kwenda akaunti zao za m-pesa kwani huduma ya kadi za mastercard inafikia ukomo.

Hata hivyo jambo la kufurahisha ni kuwa, Vodacom wamekuja na huduma ingine ya M-Pesa VISA Card kama mbadala wa huduma iliyofikia ukomo.

voda visa ujumbe

M-Pesa VISA Card ni Virtual debt card (kama kadi zile za benki) inayokuruhusu  kufanya miamala mtandaoni. Tofauti yake ni kuwa yenyewe haishikiki na unaweza kuitengeneza au kuiondoa muda wowote unaohitaji. Pia mitandao mingine ya simu inayotoa huduma za kifedha kama Airtel Tanzania wana huduma kama hii.

Kama utapenda kutengeneza kadi yako mpya ya VISA Card kwa ajili ya kufanya manunuzi mtandaoni au kulipia huduma mbalimbali mtandaoni basi fuata hatua zifautazo hapa chini.

kupitia simu yako ya mkononi (janja au kitochi) nenda sehemu ya kupigia kisha;

  1. bofya *150 *00 #
  2. halafu namba 4 (Lipa kwa Mpesa)
  3. kisha namba 6 (M-Pesa VISA Card)
  4. mwisho chagua namba 1 (Tengeneza Kadi)

Baada ya hapo utapokea ujumbe mfupi wa maneno wenye maelekezo yenye namba za kadi yako, namba 3 za CVV pamoja na muda wa matumizi ya kadi husika. Kumbuka taarifa hizi ni za siri unatakiwa uzihifadhi kwa umakini kwani mtu mwingine akizipata anaweza kuzitumia kufanya miamala bila ridhaa yako.

Habari bado inaendelea kuongezewa…

Endelea kuwa nasi kupitia mitandao ya kijamii, na channel yetu ya youtube

Mwandishi Alice Mhariri Mkuu
Mitandao ya Kijamii
Alice ni mwandishi na mhariri wa makala mbalimbali hapa Mtaawasaba tangu mwaka 2016. Akiwa hayupo kazini hupendelea kusoma vitabu, kuogelea na kusikiliza muziki
2
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive