Vigezo na Masharti

Vigezo hivi vilihaririwa mara ya mwisho: Februari 1, 2022 (angalia matoleo yaliyohifadhiwa)

TOVUTI HII NA HUDUMA ZINGINE ZENYE UHUSIANO NAYO VINAGUSWA NA VIGEZO NA MASHARTI HAYA. TAFADHARI SOMA TAARIFA HII KWA UMAKINI MKUBWA. KUENDELEA KUTUMIA TOVUTI HII ITAMAANISHA KUWA UMEKUBALIANA NA VIGEZO NA MASHARTI KAMA YALIVOORODHESHWA HAPO CHINI. KAMA HUKUBALIANI NA MASHARTI HAYA, TAFADHARI ONDOKA SASA IVI.

Vigezo hivi vinaigusa kila tovuti, tovuti ya rununu, app, na/au huduma zingine, bila kujali jinsi zinavyosambazwa, kuchapishwa au kutangazwa na Mtaawasaba, kampuni mama, kampuni dada au washirika wetu ambao wanaguswa na makubaliano ya mtumiaji na sera za faragha, ambazo zinawabana wote wanao fikia, tembelea na/au kutumia huduma, iwe mtu binafsi au kwa niaba ya kikundi, ikiwemo wewe na watu wengine, injini za kidijitali za namna yoyote zinazopekua, vuta, sambaza taarifa zetu. Utaruhusiwa tu kutumia taarifa zetu kama hazitatumika katika vitendo vya kihalifu ama namna yoyote iliyokatazwa na masharti yetu


Nakala za Vigezo na Mabadiliko

Mtaawasaba inaweza badili Vigezo hivi, kwahiyo tunakushauri uwe unapitia ukurasa huu mara kwa mara. Toleo jipya kabisa la Vigezo hivi (pamoja na tarehe vilipoanza kutumika) vitaunganishwa kwenye tovuti zetu zote ambazo vigezo hivi vinazihusu. Kama utaendelea kutumia tovuti ya Mtaawasaba na huduma zingine baada ya mabadiliko ya vigezo, utakuwa umekubaliana na mabadiliko hayo. Unaweza kuchapisha/kudurufu nakala ya Vigezo hivi na masharti kwa kutumia kitufe cha kuprint kwenye kisakuzi unachotumia. Tunashauri uhifadhi nakala yako ya vigezo hivi na masharti.


Sera ya faragha na vigezo vingine

Sera zetu za faragha zinaelezea ni nini tunafanya na taarifa unazotupa au tunazokusanya kuhusu wewe kupitia tovuti na huduma zetu zingine, kama utaruhusu taarifa zako zitumike katika mtandao wetu.

Zaidi, sera hizi zinaweza kuhusu baadhi ya sehemu ya tovuti au huduma zetu. Ikitokea hivyo basi tutaziweka sera hizi katika tovuti ama huduma husika, ambapo zitaonesha kutokea kwenye sera hizi hapa. Kama kutakuwa na mkanganyiko kati ya sera hizi basi kutakuwa na sera zingine zitakazotumika kwenye tovuti ama huduma husika pekee.

Mashindano au zawadi ambazo zitatolewa kwenye tovuti ya Mtaawasaba au huduma zetu zingine, kunaweza kuwa na sheria na mahitaji mengine kama vile umri, eneo na kuelewa, kuwa tayari kukubali vigezo na masharti ya shindano husika.


Kujiunga na udhibiti wa taarifa

Ni jukumu lako kuhakikisha usiri wa jina lako la mtumiaji na nywila yako na unakubali majukumu yote yanayoambatana na matumizi ya jina lako la mtumiaji, mashtaka, au uharibifu utakaotokea kwenye akaunti yako. Kama una sababu yoyote inayokufanya uamini akaunti yako inatumiwa na mtu mwingine bila ridhaa yako, wasiliana nasi mara moja. Hatutahusika kwa namna yoyote kuhusiana na upotevu wa taarifa zako au uharibifu utakaotokana na wewe kushindwa kutupa taarifa kuhusiana na matumizi mabaya ya akaunti yako.

Tukiomba taarifa zako binafsi wakati wa kujiunga, tunatarajia utatupa taarifa sahihi na za uhakika na utaziboresha pale itakapolazimu. Ni wajibu wako kuzirekebisha au kuboresha taarifa zako ili ziendelee kuwa sahihi, kamili na za uhakika kwa kipindi chote. Tuna uwezo wa kukubali au kukataa ombi la kujiunga au kuondoa uanachama wako kwenye mtandao wetu au huduma zetu muda wowote kwa taarifa au bila kukutaarifu. Hautaruhusiwa kufikia maeneo yanayofikiwa kwa umri kama haujafikia umri husika.


Hakimiliki

Vyote vilivyomo kuanzia taarifa, data, muonekano na mengine yote yanayohusiana na tovuti na huduma zetu zingine yanalindwa na sheria ya hatimiliki. Utatakiwa kukubaliana na sheria zote za hatimiliki na makatazo mengine. Alama zote, huduma, nembo zilizotumika kwenye tovuti hii ni mali ya wamiliki wake.

Kutokana na vigezo hivo, unakubali kutumia tovuti hii na huduma zake kwa matumizi binafsi na sio kibiashara. Tunabaki kuwa na haki ya machapisho yote katika tovuti hii, huruhusiwi kunakili, kudurufu, kusambaza, kuchapisha, kuonesha au kuboresha kazi za tovuti hii na huduma zingine bila ruhusa.

  1. Leseni za biashara

Utahitajika kupata ruhusa ya maandishi ya kutumia machapisho ya Mtaawasaba kwenye tovuti ama huduma zingine. Kama unataka kupata ruhusa ya kutumia, tafadhari wasiliana nasi kupitia [email protected]


Malalamiko ya kisheria

Kama unaamini kuna chapisho kwenye tovuti au huduma zetu linakiuka hakimiliki yako au ya watu wengine, tafadhari wasiliana nasi kupitia [email protected]. Kama una malalamiko ya kisheria zaidi ya hakimiliki basi tuandikie kupitia [email protected]

Vigezo na Masharti

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive