Kama umeshasajiliwa na mamlaka ya vitambulisho ya taifa (NIDA). Ila kwa namna moja au ingine haujapata kitambulisho chako cha utambulisho wa taifa usihofu. hapa tutakuchambulia Jinsi ya kupata namba ya nida mtandaoni (2022) hata kama hujapata kitambulisho bado.
Jinsi ya kupata namba ya NIDA mtandaoni (2022)
Njia hii inahitaji uwe una simu au kifaa kama kompyuta ambacho kimeunganishwa mtandao wa intaneti ili uweze kufanikisha zoezi hili. Kama jibu ni ndiyo basi fuata hatua hizi hapa chini na utapata namba yako ya Nida
- Fungua tovuti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
- Kisha chagua link ya National Identity menu au nenda moja kwa moja kwa kutumia anwani hii NIDA Online-Services
- Ukurasa utakutaka uandike majina yako kamili
- Jaza tarehe ya kuzaliwa
- Andika majina ya mama yako (kama ulivyoandika wakati wa usajili)
- Bofya Search.
Sekunde kadhaa utaletewa namba yako ya kitambulisho wa kitaifa. Kama utakuwa umekosea kujaza taarifa, mfumo utakutaka ujaze upya kwa usahihi kisha utafute tena.
Jinsi ya kupata namba ya nida kwa kutumia USSD (Simu za kiganjani)
Kama hauna mtandao wa intaneti ila unasimu ya mkononi inayotumia mtandao wa Vodacom au Airtel basi unaweza pata namba yako ya nida kwa kutumia ussd code. Fuata hatua zifuatazo
- Andika *152*00#
- Kisha andika 3
- Chagua 2
- Andika Majina yako matatu (la kwanza, kati na ukoo mfano; Shaban Juma Mzee)
- Andika namba ya simu uliyotumia wakati wa usajili
- Kubali kulipa gharama zitakazotozwa kwa huduma hii
Baada ya sekunde kadhaa utapokea ujumbe mfupi ukiwa na namba yako ya kitambulisho cha NIDA. Kama utakuwa umeingiza taarifa kimakosa utatakiwa kuanza upya huku ukiingiza taarifa kwa umakini.
Jinsi ya kupata namba ya nida kupitia ofisi za NIDA za mkoa
Hii ni njia ya mwisho, ambayo inabidi kama njia za mwanzo zimeshindikana kabisa kupata namba ya kitambulisho ya NIDA. Fika ofisi ya mkoa iliyokaribu na wewe kisha waelezee hitaji lako la kutaka kupata namba ya NIDA na watakusaidia.
Unaweza [irp posts=”25284″ name=”Jinsi ya kupata TIN number mtandaoni”]