Google Pixel Watch iliyosubiriwa kwa muda mrefu hatimaye ilitangazwa katika Google I/O ya mwaka huu, ingawa kampuni hiyo haikutoa maelezo mengi kuhusu bidhaa zilizotangazwa siku iyo. Ni muda sasa kumekuwa na tetesi za Google kuja na saa janja yake, tetesi hizo zilianza kuwa na dalili ya ukweli baada saa iliyodhaniwa kuwa ni Pixel Watch kuonekana kwenye mgahawa mmoja siku kadhaa kabla ya Google I/O. Taarifa zaidi zinadai saa hii itapewa nguvu na chipset ya Exynos na betri yenye ukubwa wa 300 mAh. Na sasa kuna taarifa za majaribio ya ndani kuwa Betri ya Google Pixel Watch inaripotiwa kudumu kwa siku moja.
Kwa mujibu ya ripoti iliyochapishwa na 9to5Google, zikinukuu chanzo kutoka ndani ya kampuni zinadai betri ya saa janja hii itadumu kwa siku moja pekee, haijasemwa ni katika mazingira yapi, je kipengele cha always on display kinakuwa kimewashwa siku nzima au la, pia haijasemwa kama inajumuisha mchana na usiku au lah. Saa janja nyingi zinazotumia mfumo endeshi wa Wear OS uwa zina betri dhaifu ila zinaweza kushinda siku nzima na usiku kucha, wakati mwingine hufika hata jioni ya siku inayofuata kabla ya kuchajiwa tena.
Ripoti hii ya 9to5Google inazidi kusema, sio tu kwamba maisha ya betri hayatakuwa makubwa bali uwezo wa kuchaji saa janja hii nalo ni tatizo lingine kwani, Google Pixel Watch haina uwezo wa kuchaji kwa kutumia wireless dock za USB-C. Hii ina maanisha saa itachajiwa polepole sana ukilinganisha na saa janja jama Apple Watch 7 ambayo itajaa chaji ndani ya dakika 75 tu. Kwaiyo sasa fikiria utatakiwa usubiri hadi dakika 110 (kwa mujibu wa ripoti) kuchaji Google Pixel Watch kisha uitumie kwa muda usiozidi siku moja.