- Ramani, StartUp kutoka Tanzania inayoangazia minyororo ya usambazaji wa bidhaa zilizofungashwa na walaji (CPG), imepanga kuanzisha huduma mpya za kifedha wakati ikipanua shughuli zake katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki baada ya kukusanya dola milioni 32 katika duru ya usawa wa madeni ya Series A.
Ramani, kampuni yenye makao makuu yake nchini Tanzania, imejikita kwenye kujenga mtandao wa vituo vidogo vya usambazaji wa bidhaa zenye thamani ya dola trilioni moja barani Afrika, imekusanya dola za Marekani milioni 32 za ufadhili.
Ramani, kutoka Tanzania yakusanya $32m
Kampuni hii ambayo ilianzishwa mwaka 2019 na ndugu wawili Iain Usiri, na Calvin Usiri, pamoja na Kibet Martin, inajihusisha na mnyororo wa usambazaji wa bidhaa zinazotumiwa na mlaji (consumer). Kampuni hii inatatua changamoto ya upatikanaji wa taarifa na vituo. Ramani, kwa kutumia teknolojia ya kisasa inatengeneza mifumo ya usimamizi wa hesabu, na huduma za ugavi, na programu za kuuzia (Point of Sales) ili kufanya mchakato mzima wa ugavi kuwa kidijitali zaidi.
Ramani wanasema, jukwaa lake lina zaidi vituo 100 vidogo vidogo vya usambazaji, na wanatarajia idadi hii kukua kwa kasi kwani wanaongeza maradufu shughuli zao nchini Tanzania na kuanzisha huduma mpya. Kwa sasa Ramani ina ingiza mapato ya ujumla kiasi cha dola za marekani milioni 72 kwa mwaka. Washirika wake wakubwa ni pamoja na makampuni ya vivywaji kama kampuni ya Coca-Cola, Mega Beverages, Hill Water, Tanga Fresh na Serengeti Breweries, kampuni ya mafuta na gesi kama Shell, Puma Energy na Oryx bila kusahau Dangote Group.
Duru ya hivi karibuni ya ufadhili wa Ramani ni sehemu ya mwenendo wa kuongeza uwekezaji katika kampuni za teknolojia nchini Tanzania. Kwa kiasi kikubwa, Ramani imeeleza kuwa ina mpango wa kushiriki Silicon Zanzibar, mpango wa umma na binafsi unaolenga kujenga kitovu cha kampuni za teknolojia za Kiafrika visiwani Zanzibar, ikiwa ni pamoja na marupurupu kama vile msamaha wa miaka 10 kutoka kwa kodi ya kampuni. Mradi huo unaongozwa na Wizara ya Uwekezaji na Maendeleo ya Kiuchumi Zanzibar pamoja na majukwaa ya kidijitali ya Kenya ya Wasoko na Tushop.