YouTube kuongeza nguvu kuzuia wanaotumia Ad Blocker

Alice Maoni 167

YouTube kuongeza nguvu kuzuia wanaotumia Ad Blocker ku-block matangazo ya YouTube.

Taarifa hii ilianza kusambaa kwa mara ya kwanza na mtumiaji wa Reddit wiki hii, YouTube imeonyesha onyo la pop-up baadhi ya watumiaji kwamba “Ad-Blockers haviruhusiwi.”

YouTube huweka matangazo mengi na yasiyokwepeka kwa njia ya kawaida, hali hii hupelekea watumiaji wengi kutumia Ad Blockers au app ambazo zinaweza kuchuja na kuzuia matangazo ya YouTube. Idadi ya watu ambao wanatumia Ad Blockers inaongezeka kila mwezi na kila mwaka.

Ili kukwepa matangazo ya YouTube ni kulipia huduma ya kulipia ya YouTube Premium. Google imekuwa ikiruhusu matumizi ya Ad-Blocker na programu za kuchuja matangazo kwa muda sasa, hata hivyo siku za karibuni imekuwa ikifanya mpango wa kuweka mfumo mpya ambao utakuwa unazuia Ad Blockers na kuzuia watazamaji ambao wanatumia app na extensions za kuzuia matangazo ya YouTube.

Watumiaji wa YouTube ambao wanapenda kublock matangazo wameongezeka sana na idadi kwa sasa ni kubwa na inapelekea YouTube na watengeneza maudhui kukosa faida.

Kwa sasa itakuwa ukitumia programu za kuzuia matangazo utaletewa ujumbe ambao unakuambia Ad Blockers haziruhusiwi YouTube. Pia kuna maelekezo yanayoonyesha kujiunga na YouTube Premium ili kutazama bila matangazo na maandishi ya kusisitiza kuwa unapotumia Ad Blocker unaongeza gharama za uendeshaji wa YouTube kuendelea kupatikana bure na content creators kupata faida.

YouTube kuongeza nguvu kuzuia wanaotumia Ad Blocker

Majaribio haya yameanza wiki hii kwa baadhi ya watumiaji, tutegemee kuona YouTube inaanza kuweka mabadiliko haya rasmi kwa watumiaji wote duniani.

Mwandishi Alice Mhariri Mkuu
Mitandao ya Kijamii
Alice ni mwandishi na mhariri wa makala mbalimbali hapa Mtaawasaba tangu mwaka 2016. Akiwa hayupo kazini hupendelea kusoma vitabu, kuogelea na kusikiliza muziki
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive