Mkutano mkubwa wa WWDC 2023 sasa umeisha na kupitia chapisho hili tuna kuangazia matangazo yaliyojiri. #Apple ilitangaza masasisho kwa mifumo yake yote ya sasa ya uendeshaji, pamoja na mfumo mpya wa uendeshaji wa visionOS. Kwa kuongezea, kampuni hiyo imetangaza Mac kadhaa mpya na gajeti ya kuvaa kichwani ya Vision Pro.
#WWDC2023 ilifanyikia Apple Park huko Cupertino, California, Marekani. kwenye Tukio la mseto lililokuwa na ma developer na watu kutoka kwenye vyombo vya habari waliohudhuria hafla hiyo kibinafsi. Haya hapa matangazo yote yaliyotolewa wakati wa WWDC 2023 keynote.
Kila kitu kilichotangazwa kwenye Apple WWDC 2023
15-inch MacBook Air
Apple ilizindua MacBook Air ya inchi 15 kwa $ 1,299. Kifaa hiki kinakuja na chip ya M2, ambayo, kulingana na Apple, ina CPU yenye kasi zaidi 18% na GPU ya kasi ya 35% kuliko mtangulizi wake. Katika mfano wa msingi, utapata CPU ya core 8 na GPU core 8, lakini unaweza kuboresha ili kupata GPU ya core 10 badala yake, ikiwa unataka kuongeza utendaji kidogo katika upande wa picha. Pia ina 8GB ya RAM, lakini unaweza kuboresha hadi 24GB. Inatoa hadi masaa 18 ya maisha ya betri.
Mac Studio na M2 Max na M2 Ultra
Mac Studio na M2 Max ina matobo mawili ya USB-C kwa mbele, wakati Mac Studio na M2 Ultra ina matobo mawili ya Thunderbolt 4. Apple pia imeweza kuweka matobo ya SD kadi yanayopangwa mbele ya mashine. Kwa upande wa nyuma kuna matobo manne ya Thunderbolt 4, mawili ya USB-A, Ethaneti ya 10Gb, HDMI, na audio jack.
M2 Max inakuja na CPU yenye core 12 na GPU core 30 na msaada wa hadi 96GB ya RAM, kasi yake ni 25% haraka kuliko M1 Max. M2 Ultra, kwa upande mwingine, inakuja na mara mbili specs hizi na CPU core 24, GPU core 60, na hadi 192GB ya RAM.
Mac Studio inaingia sokoni kuanzia leo unaweza kuweka oda yako.
Mac Pro na M2 Ultra
Apple ilitangaza Mac Pro na M2 Ultra. Hii Ina matobo 8 ya Thunderbolt na nafasi 4 za PCI kwa upanuzi. Mac Pro ina kasi hadi 3x haraka kuliko kizazi cha awali cha Intel. Ikiwa na hadi 192GB ya kumbukumbu iliyounganishwa RAM, Mzigo unaingia sokoni kwa bei ya $ 6999. unaweza kuweka oda sasa
iOS 17 yalenga vipengele vya mawasiliano
Apple pia imetangaza iOS 17, Sasisho hili la mfumo limejikita zaidi kwenye vipengele vya mawasiliano.
- Kipengele kipya cha AirDrop kinachoitwa NameDrop kitakuruhusu kusambaza kwa urahisi na bila tatizo nambari yako ya simu, na hata picha, na mtu mwingine. Hivi ndivyo inavyofanya kazi: Unapoleta simu zako karibu, unaweza kuchagua kusambaza nambari yako ya simu na anwani ya barua pepe. Unaweza kutumia NameDrop na iPhone na Apple Watch pia.
- Apple inaanzisha programu mpya ya uandishi wa habari inayoitwa Journal. Kutumia ujifunzaji wa mashine ya vifaa, iPhone itakupa maoni binafsi kuhusiana na picha zako, shughuli, eneo, muziki, mazoezi, nk.
- Upande wa autocorrect, Apple wameboresha autocorrect, sasa itasaidia na akili za bandia kujifunza maneno unayotumia mara kwa mara ili kuweza kukupa mapendekezo.
- Mabadiliko mengine ambayo hakuna aliyetegemea kwenye iOS 17: Apple wameondoa neno “hey” kwenye “Hey Siri.”
Unaweza kusoma zaidi kuhusu iOS 17 hapa.
iPadOS 17 na maboresho ya vipengele kwenye iPad
Ukiwa na iPadOS 17, Apple wameleta maboresho ya lock Skrini, pamoja na PDF autofill, na vipengele vya iOS 17, kama vile uwezo wa kurekodi video ikiwa mtu hapokei simu yako. Kwa kuongezea, iPadOS 17 imewekewa programu ya Afya kwa mara ya kwanza.
Mifumo endeshi mingine iliyoachiwa ni pamoja na;
macOS 14 Sonoma
tvOS 17
watchOS 10
watchOS 10 inakuja na maboresho na makubwa kwa programu zake na vipengele ikiwemo:
- maboresho ya muonekano wa saa
- kitufe cha kidijitali kinachozunguka kusogeza wijeti
- Muonekano mpya wa saa
- Pallet and Snoop are among the two new Watch Faces
wanaofanya mazoezi na wanaotembea, zimeongezwa taarifa zaidi kuhusu wanachofanya - ramani zitaanza kuonekana kwenye saa, kwa kuanzia wanaanzia Marekani
visionOS
visionOS huu ni mfumo endeshi mpya kwa ajili ya kifaa kinachovaliwa kichwani cha vision Pro, unaofanana na iOS kimuonekano kwa baadhi ya programu unazozifahamu na kuzipenda.
Baadhi ya programu utakazopata kwa sasa kwenye mfumo endeshi huu ni pamoja na Safari, Calendar, Contacts, Mail, Messages, Freeform, Photos, na zaidi.