Blackberry, moja ya kampuni iliyotengeneza simu zilizojizolea umaarufu mkubwa miaka ya nyuma, imetangaza kuwa Simu zinazotumia Blackberry OS kuacha kufanya kazi kuanzia Januari 4 mwaka huu 2022.
Taarifa hii ya kusitisha kufanya kazi kwa simu zote zinazotumia mfumo endeshi wa Blackberry Os unahusisha simu zote zenye mfumo wa Blackberry 7.1 na kurudi nyuma, hata hivyo vifaa vyenye Blackberry 10 na Blackberry Playbook OS 2.1 kurudi nyuma zitapoteza uwezo muunganisho wa WI-Fi kufanya kazi kama kawaida.
Vifaa hivi vitakosa uwezo wa kupata masasisho ya moja kwa moja na huduma zingine za namna hiyo ikiwemo uwezo data, kupiga na kupokea simu, na uwezo wa simu za dharura polisi 991. Pia huduma za BlackBerry Link, BlackBerry Desktop Manager, na BlackBerry Blend hazitaweza fanya kazi kama kawaida.
usitishwaji wa huduma na miundombinu hii pia itaathiri ufanyaji kazi wa pp zingine kama Enhanced Sim Based Licensing (ESBL) / Identity Based Licensing (IBL), BlackBerry hosted email addresses, BlackBerry Link, BlackBerry Desktop Manager, BlackBerry Blend, BlackBerry Protect (inayowezesha mtumiaji kuifunga simu, kutafuta au kufuta data za BlackBerry OS, na BlackBerry 10 bila kuwa na simu.
huduma zingine za ulinzi wa artificial intelligency hazitaathirika na usitishwaji huu wa huduma.
Simu na vifaa vingine vya Blackberry vinazotumia mfumo endeshi wa Android havitaathirika na usistishwaji huu wa huduma, isipokuwa huduma ya barua pepe iliyoelekezwa kwenye anwani za barua pepe zinazosimamiwa na Blackberry au ambazo zinatumia huduma ya ESBL na IBL.
kufuatia mwisho wa huduma hizi, watumiaji wa huduma za barua pepe zinazosimamiwa na Blackberry watalazimika kuhamia kwenye barua pepe mpya. Kwa wanaotumia vifaa vya iOS au Android na wanatumia huduma zilizokuwa zinapewa leseni na Blackberry watalazima kupata leseni mpya kwa mifumo wanayotumia.
Kwa wale ambao bado wanatumia vifaa vyenye Blackberry Os wanaweza kutembelea ukurasa wa BlackBerry’s FAQ section ili kupata ufafanuzi wa maswali yawaliyo nayo.
Mwaka 2015, Blackberry waliacha kutengeneza vifaa vinavyotumia Blackberry OS na kuhamia kwenye mfumo endeshi wa Android kwenye simu na tableti zao.
Miaka ya karibuni kampuni ya Blackberry imehama katika kutengeneza vifaa kama simu na tableti na kujikita zaidi kwenye utengenezaji wa software hasa hasa software za ulinzi na huduma kwa mashirika makubwa na serikali mbalimbali duniani