Facebook sasa ina programu ambayo inaruhusu watu katika nchi zinazoendelea kupata location na kulipia Wi-Fi. Kampuni hiyo ilizindua programu ya Facebook Express Wi-Fi inayopatikana kwenye Google Play Store kwenda pamoja na mtandao wa Wi-Fi iliyogawanywa. Kwa sasa programu hiyo inafanya kazi tu Indonesia na Kenya.
Programu hii hutoa watumiaji njia ya kupata maeneo ya karibu zaidi ya Wi-Fi na kuweza kununua vifurushi vya data. Hapo awali kuipata Facebook Express Wi-Fi, watumiaji wangepaswa kufungua kivinjari cha simu ya mkononi au kupakua programu kutoka kampuni ya simu ambayo inaweza kuwauliza upya mipangilio ya simu zao. Njia hii pia itaweza kuwapa watumiaji kujua mahali ambapo hotspots au Public Wi-Fi zinakopatikana.
“Facebook inatoa programu ya Express Wi-Fi katika duka la Google Play ili kuwapa watu njia nyingine rahisi na salama ya kufikia mitandao kwa haraka na kwa bei nafuu kupitia maeneo ya ndani ya Wi-Fi ya Express,” kampuni hiyo imesema.
Wakati programu hii ikiwa inapatikana na kufanya kazi katika nchi mbili tu kwa sasa, Express Wi-Fi tayari iko katika nchi tano kuweza kutumika zikiwemo: India, Kenya, Tanzania, Nigeria, na Indonesia. Inategemea wamiliki wa biashara wanaoendesha maeneo yao ya Wi-Fi ambayo watu wa karibu wanaweza kulipa kufikia bandwidth ya kasi ya juu kwa kutumia ISP za mitaa, ikilinganishwa na uhusiano wa kawaida wa simu.
Express Wi-Fi imekuwa jaribio jingine kutoka Facebook ili kuleta internet kwenye nchi zinazoendelea, unaweza ipakuwa Programu hiyo kupitia hapa