Facebook ina mpango wa kuboresha News Feed ili kukuza habari muhimu

Diana Benedict Maoni 152

Facebook imetangaza kufanya kile inachokiita kuwa ni mabadiliko muhimu ambayo itafawafanya watumiaji wa tovuti hiyo kuwa na mawasiliano yenye umuhimu zaidi katika maisha yao ya kila siku.

facebook

Watu watapata habari zaidi juu ya marafiki zao na familia na taarifa juu ya makampuni na taasisi zitapungua kwenye mtandao huo.Mkurugenzi mkuu wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg ameeleza kuwa maudhui ya biashara na vyombo vya habari yalikuwa yanamuondoa mtu katika nyakati muhimu ambayo watu wengi wanaithamini zaidi.

“Ni jukumu letu la kuhakikisha huduma zetu sio furaha tu kutumia kwa watumiaji wetu , lakini pia ni nzuri kwa ustawi wa watu,” Mkurugenzi Mtendaji Mark Zuckerberg alisema

images

Amesema vipaumbele ambavyo Facebook imeviweka ili kuondoa changamoto iliyopo inaweza kumaanisha kuwa watu watatumia muda mfupi zaidi katika mtandao huo ,lakini muda ambao watautumia utakuwa na thamani kubwa zaidi.

Haya yakiwa mabadiliko mamkubwa katika mtandao huo wenye watumiaji zaidi ya bilioni mbili duniani kote,itaongeza mapato kutoka kwenye matangazo.

Licha ya kuwa ,Facebook imekuwa katika shinikizo kubwa la kukabiliana na watu ambao wamekuwa wanapenda mtandao huo kupita kiasi ambacho wanaweza kuatharika na afya ya akili.

Mwandishi Diana Benedict Mwandishi
Mitandao ya Kijamii
Diana Benedict. Digital Creator | IT Specialist | Graphics Designer | Web Designer | Web SEO | Contents Management | UI/UX Designer and Social Media Management.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive