Wakati kampuni za Samsung na Apple zikiwa zimezindua simu zake mwanzoni mwa mwezi wa tisa, Google inatarajia kuzindua simu mbili mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2017.
Mwaka 2016, Octoba 4 Google iliacha kutumia brand name ya simu zake za zamani Google Nexus na kuanza kutumia Brand Name ya Google Pixel na Google Pixel XL na kuziingiza sokoni, kutokana na device hizo kufanya vizuri, Kampuni ya Google inatarajia kuzindua Google Pixel 2 na Google Pixel XL 2.
Muundo wa simu hizi mbili zinatarajiwa kufanana na Simu za Samsung S8, Note 8 na iPhone X. Kupitia ukurasa wa Android Authority simu hizi zitakuwa Manufactured na Kampuni ya LG kwa Google Pixel XL 2 na HTC kwa Google Pixel 2.
Tufuatilie @MtaaWaSaba kwenye Twitter, Facebook, instagram, Google+ na YouTube kwa habari zaidi, Pia usisite kututumia maoni yako [email protected]