Mwanzoni mwa mwezi wa tisa mwaka huu kampuni ya Samsung ilizindua simu yake aina ya Samsung Galaxy Note 8.
Nimekusogezea hapa uweze kuitambua kiundani Zaidi simu hii mpya kutoka Samsung.
Muonekano;
Samsung Galaxy Note 8 imeundwa kwa Aluminum pembeni yake na yenye umbo la kioo kigumu katika shepu yake ya nyuma, kwa sasa Samsung Galaxy Note 8 inapatikana katika rangi nne (Midnight Black, Maple Gold, Orchid Grey na Dark Blue).
Samsung Galaxy Note 8 ina uzito wa gramu zisizopungua 195g na umbo la milimita mstatili wa 162.5mm Urefu, 74.8mm Upana na wembaba wa 8.6mm, Pia Samsung Galaxy Note 8 imeongezwa baadhi ya vipengele katika Device yake kwenye S-Pen na kwa sasa unaweza kukopi na kuchora au kupiga screenshot eneo unalolihitaji tu katikia screen unayotumiakwawakati huo.
Display;
Samsung Galaxy Note 8 ina ukubwa wa inchi 6.3”(Infinity Display), Kioo kikubwa kilichochukua zaidi ya 83.2% ya umbo zima la simu, na resolution ya 1440 x 2940 Pixel. Pia Samsung Galaxy Note 8 imeundwa kwa kioo kigumu amabacho si rahisi kupasuka kwa kuangushwa kwa kawaida.
Camera;
Samsung Galaxy Note 8 ina kamera mbili (Dual Camera) zenye uwezo wa Megapixel 12MP kila moja (26mm, f/1.7, PDAF & 52mm, f/2.4, AF) na yenye mwanga Zaidi kwenye flashilight kwa kurekodi matukio ya usiku,pia katika video unaweza kurekodi hadi kufikia 2160P (4k), 1080P, na 720P.
Kwa kamera ya mbele Samsung Galaxy Note 8 inaukubwa wa Megapixel 8MP,f/1.7kwa ajili ya video call na selfie. Tunaopenda selfie simu hii ni nzuri sana kutumia.
Software, Hardware Specification;
Samsung Galaxy Note 8 inakuja na Android 7.1.1 (Nougat) Pre-installed, na utaweza ku-update hadi Android 8.0 (Oreo) inayotarajiwa kutoka siku chache zijazo.
Samsung Galaxy Note 8 ina Octa core (4×2.3GHz na 4×2.35GHz) Exynos Processor 8895 Octa-EMEA,Qualcom Snapdragon 835, na ina GPU ya Adreno 540. Samsung Galaxy Note 8 ina nguvu ya kushika mawimbi ya GSM, HSPA (3G) na 4G LTE speed Zaidi ya 150Mbps download speed, dual Wi-Fi 802.11, Bluetooth 5.0 A2DP, EDR, LE yenye uwezo Zaidi.
Storage na Bettery;
Samsung Galaxy Note 8 zina ukubwa wa 256GB, 128GB na 64GB zenye uwezo wa 6GB RAM. Battery ya Samsung Galaxy Note 8 ina ukubwa wa 3300mAh, ina uwezo wa kukaa Zaidi ya masaa 22 kwa kuongeana simu kwenye mtandao wa 3G, Zaidi ya masaa 74 kwa kucheza Music na Zaidi ya masaa 89kwa standby mode.
Hitimisho;
Samsung Galaxy Note 8 inapatikana katika maduka yote ya Samsung Tanzania, na Inatazamiwa kuuzwa kati ya TzSh. 2,285,000/=.
Usisite kutuachia maoni yako hapo chini pia tutembelee katika Social Network @MtaawaSAba katika Facebook, Twitter, Instagram, Google+ na YouTube. Tuandikie maoni yako [email protected]
Comment:duuuh hela ndefu
Nomaa