Kuhusu sisi

Sisi ni nani

Mtaawasaba ni blogu mahususi kwa ajili kila kitu kuhusu teknolojia. Ni imani yetu utapenda machapisho yetu na utajiunga nasi ili usipitwe kila tunaotoa habari mpya.
Tangu mwaka 2012 tulipoanza, Mtaawasaba imekuwa ni chanzo cha kuaminika cha habari, matukio, tafiti, video,  uchambuzi wa kina unaohusu maswala ya teknolojia na ugunduzi bila kusahau maujanja mbalimbali. Tunahakikisha machapisho yetu yanapitiwa na wahariri wetu kabla hayajakufikia msomaji wetu mpendwa. Lengo letu ni kukupa habari, kukuunganisha na kukusimua.

Timu yetu

Waandishi

  • Joeli, Muanzilishi na msimamizi wa karibu kila kitu
  • Kato Kumbi, Mwandishi mkuu na msimamizi
  • Emmanuel Tadayo, Mwandishi
  • Hemedans Nassor, Mwandishi
  • Hassan Kabelwa, Mchangiaji

Kama unadhani unaweza kuandika kwa ajili ya Mtaawasaba, usisite bofya hapa kuwasiliana nasi

 

Historia

Tovuti hii ilianzishwa Novemba 2012 na Joeli, mshabiki na mwandishi wa maswala yahusuyo teknolojia. Ilianza kufanya kazi rasmi mwaka 2013 mwezi wa pili.

Mtaawasaba.com na Mtaa.ws ni mali ya Mtaawasaba Media.

Unahitaji kuwasiliana nasi?

Tunapenda kusikia kutoka kwako msomaji wetu. Una taarifa unataka kutupa? Maswali au maoni kwa timu ya Mtaawasaba? Tuandikie kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano ili utoe yako ya moyoni.

Matangazo, Leseni, na Ruhusa kutumia machapisho?

Kama unapenda kutangaza kupitia Mtaawasaba.com ama unahitaji ruhusa kutumia machapisho yetu, tafadhari wasiliana nasi kupitia ukurasa wa ruhusa na matangazo.

Ungependa kuwa mwandishi wa Mtaawasaba?

Kama unaamini una uwezo wa kuandika vizuri kuhusu teknolojia hasa kuhusu gajeti, softiwea na mengine yahusuyo teknolojia, kwa nini usifikirie kuwa sehemu ya timu ya Mtaawasaba?

Masharti na vigezo vyetu hata sio vigumu, cha muhimu uwe unaweza kuongea na kuandika kwa kiswahili fasaha.

Sera yetu ya faragha

Unaweza kusoma sera yetu kuhusu faragha yako msomaji wetu hapa