Ni muda sasa kumekuwa na tetesi ambazo zimekuwa zikigonga vichwa vya habari kuwa kampuni kubwa ya Google iko mbioni kuachia saa janja yake ambayo itaitwa Google Pixel Watch. Uvumi huu unaelekea kuwa kweli kwani kumeibuka picha halisi za saa janja inayodhaniwa kuwa ni Google Pixel Watch. Kwa mujibu ya taarifa ya mwanzo kabisa ambayo iliyoripotia na Android Central zinadai saa hiyo iliachwa na mtu mezani kwenye mgahawa mmoja huko Marekani.