Kwenye mkutano wa WWDC 2023, Apple wazindua iOS 17. Sasisho hili limejikita zaidi kwenye programu za mawasiliano, akili/uelewa na experience mpya. Hapa tunakuletea kila kitu unahitaji kujua kuhusu iOS 17
Sehemu ya kwanza ilikuwa ni kuhusu Simu, FaceTime, na Messages:
Vipengele vipya vya iOS 17
Maboresho ya Phone na FaceTime
Kuna mabadiliko kwenye skrini ya kupigia, utaweza kubadili picha na muonekano wa kila mtu unayewasiliana kwenye simu kadri unavyopenda
Pia iOS 17 itakuwezesha kuacha voicemaill kupitia FaceTime kama simu yako haitapkelewa, hii imekaa poa eeeenhe? mwenyewe nimeilewa.
Messages
iOS 17 inaongeza mbwembwe zaidi kwa kuleta live stickers kwenye upande wa messages. iMessages itapata muonekano mpya kwenye baadhi ya vipengele vyake.
Urahisishwaji wa Sharing
Sasa utaweza ku share majina na taarifa zingine kwa urahisi kupitia kipengele kipya cha NameDrop ambacho kinafanana na AirDrop ila chenyewe hakitahitaji muunganisho wa intaneti
Journal App
Hii ni programu mpya itakayokuwa ikikusanya taarifa mbalimbali kwenye simu kuhusu kumbukumbu mbalimbali kisha kukuletea ripoti kuhusu taarifa hizo. Taarifa hizo ni pamoja na picha ulizopiga siku fulani, utaweza pia kuongezea maneno kwenye taarifa hizo.
Standby mode
hiki ni kipengele kingine kipya ambacho kimeongezwa ambapo, simu yako ukiilaza wakati unaichaji basi itakuletea taarifa mbalimbali kuhusu kifaa chako, hali ya hewa, muda na kadhalika.
Mengineyo
- autocorrect imeboreshwa zaidi sasa itatumia akili za bandia kujua maneno unayotumia mara kwa mara ili kuweza kukamilisha sentensi unapoandika.
- Kisakuzi cha Safari kimeboreshwa, sasa utaweza kuficha baadhi ya tabs ukiwa kwenye private mode.
- Programu yaHealth inaborehswa zaidi.
- Sasa Apple Maps itakuwezesha kuitumia bila intaneti kwa baadhi ya maeneo.
- Sasa utaweza kuamsha programu saidizi ya Siri kwa kutamka neno “Siri” badala ya “Hey Siri” kama ilivyokuwa awali
- maboresho mengine mengi tutazidi kuya ainisha hapa.
iOS 17 itaanza kupatikana lini?
iOS 17 beta tayari inapatikana kwa wasanii. ila kwa watumiaji wa kawaida au ambao hawataki kufanyia majaribio mfumo endeshi huu, wanaweza kusubiri mpaka mwezi wa septemba 2023 ndiyo toleo rasmi la iOS 17 litatoka kwa watumiaji wote.
iPhones zipi zitapata iOS 17?
Simu zifuatazo ndiyo zitapata sasisho la iOS 17 baadaye mwaka huu. simu hizo ni pamoja na
2018 iPhone XS, iPhone XS Max na iPhone XR
2019 iPhone 11, iPhone 11 Pro and iPhone 11 Pro Max
2020 iPhone 12, iPhone 12 Mini, iPhone 12 Pro na iPhone 12 Pro Max
2021 iPhone 13, iPhone 13 Mini, iPhone 13 Pro na iPhone 13 Pro Max
2022 iPhone 14, iPhone 14 Plus, iPhone 14 Pro na iPhone 14 Pro Max
2020 iPhone SE 2nd Gen
2022 iPhone SE 3rd Gen
Tofauti na simu hizi, matoleo yote ya simu za iPhone 15 yatakuja na mfumo endeshi wa iOS 17.
iPhone zipi hazitapata iOS 17?
Kwa bahati mbaya iPhone 8 na iPhone 8 Plus hazitapata sasisho hili. simu ingine itakayokosa sasisho hili ni iPhone X, hii ni baada ya miaka mitano ya kupata masasisho hatimaye imefikia mwisho sasa.
iPhone X imepigwa panga muda mchache baada ya kutangazwa kwa Apple Vision Pro, kabla yake, iPhone X ndiyo ilikuwa “jambo kubwa linalofuata” kutangazwa na Apple.