NALA yapata leseni ya kutoa Huduma za Malipo Tanzania. Kuwekeza zaidi ya bilioni 2

Emmanuel Tadayo 3 161

NALA ambayo ni kampuni ya huduma za kutuma na kupokea fedha kwa njia ya kidigitali yenye makao yake makuu nchini Kenya, imepokea leseni ya Mtoa Huduma za Malipo (PSP) kutoka Benki Kuu ya Tanzania, baada ya kufanya kazi kwa karibu na wasimamizi wa fedha nchini.

Leseni hiyo kutoka Benki kuu ya Tanzania inaifanya NALA kuwa mtoa huduma ya malipo na kuwezesha muunganiko wa moja kwa moja na benki pamoja na watoa huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu za mkononi, kama vile Mpesa, Tigopesa, Airtel Money na nyinginezo.

NALA inaendeleza shughuli zake za kiutendaji nchini, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono maono ya Rais wetu, ya kujenga Tanzania iliyoinuka kiugunduzi pamoja na teknolojia kwa ujumla wake.

Akiongea na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo tarehe 27 Machi 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa NALA, Benjamin Fernandes amesema wanatarajia kufanya uwekezaji wenye thamani ya zaidi ya Bilion 2 za kitanzania ili kujenga miradi yetu mikubwa zaidi kuwahi kutokea katika soko letu la hapa nyumbani Tanzania, uwekezaji huo utaifanya NALA kuboreha huduma na kuongeza wigo wa huduma zake huku wateja wengi zaidi wakinufaika.

Fernandes amesema hatua hiyo itaiwezesha NALA kuanza kutengeneza bidhaa za ziada za kidijitali ambazo zitaongeza ujumuishaji wa malipo, kufanya huduma za malipo ziwe nafuu zaidi na za kuaminika kwa biashara na matumizi ya kawaida.

“Kwa kutumia NALA wateja wanaweza kutuma na kupokea fedha kwa nia ya kijigitali kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwa ni pamoja na Marekani, Uingereza, nchi za Jumuiya ya Ulaya na nginginezo,” amesema.

NALA imekua kwa kasi tangu kuanzishwa kwake mnamo 2018, ikitanua huduma zake hadi nchi kama Uingereza, Marekani na Ulaya. Dhamira ya kampuni hiyo ni kutoa huduma za kifedha nafuu na uwazi ili kuwawezesha watu wenye udhibiti wa fedha zao. Yote yalianza kama programu ya fedha binafsi mwaka 2018, ikiwasaidia Watanzania na Waganda kwa ustawi wao wa kifedha kabla ya kubadilika na kuwa programu yakuhamisha fedha kwa waafrika wanaoishi ughaibuni.

Kwa sasa huduma za NALA zinapatikana nchi nyingi za Ukanda wa Afrika na Ulaya, unaweza kuipakua proramu yao kwenye simu yako kupitia App Store au Play Store.

Licha ya kuwepo kwa machauo mengi ya kutuma na kupokea pesa Afrika kutoka ughaibuni, bara la Afrika bado limeendelea kuwa mahali pa gharama kubwa zaidi kutuma pesa. Benki ya Dunia inakadiria wastani wa ada za kutuma fedha Afrika kuwa 9%.

Zaidi ya hayo, machaguo mengi yanahusisha gharama kubwa za kutuma feha na  ada zilizofichwa ambazo hufanya iwe vigumu kutambua gharama halisi ya kutuma pesa. NALA inajitahidi kubadilisha dhana ya zana za kifedha kwa Waafrika kwa kutoa huduma za haki na uwazi ili kuwawezesha watu kudhibiti fedha zao.

 

Mwandishi Emmanuel Tadayo Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
mwandishi wa habari za teknolojia kwenye tovuti pendwa ya mtaawasaba
3
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive