Netflix kulipisha zaidi wanaochangia password

Emmanuel Tadayo Maoni 156

Ni ukweli usiopingika karibu kila mtumiaji wa Netflix mwenye akaunti anashea password na ndugu au marafiki. Utaratibu huu wa kushea password umekuwepo tangu kuanzishwa kwa Netflix, lakini siku si nyingi unaelekea kufikia ukomo.

Siku ya jumatano, kumekuwa na taarifa za kuwa Netflix kulipisha zaidi watumiaji wanaochangia password. Netflix wameanza kufanyia majaribio njia mpya za kudhibiti wanaoshea password, njia moja wapo inayofanyiwa majaribio ni kuwataka kulipia kama wanataka kushea password.

Taarifa hiyo inasema “kitendo cha watumiaji zaidi ya mmoja kushea akaunti kinapunguza uwezo wao (Netflix) kuwekeza zaidi kwenye michezo ya kuigiza na filamu mpya kwa ajili ya watazamaji wao”

Netflix wamesema wataanza kufanya majaribio ya mwanzo kwa nchi za Chile, Costa Rica na Peru, ambapo watumiaji watakuwa wanapata ujumbe utakaowaruhusu kuongeza watumiaji kwenye akaunti zao kwa kulipia kiasi kidogo cha fedha.

Pia watumiaji katika maeneo hayo waliolipia vifurushi vya Standard na Premium watapewa uwezo wa kuongeza akaunti ndogo ambazo zitakuwa na uwezo wa kuweka hadi watu wawili ambao hawaishi pamoja, ambao wataweza kuwa na profile zao, email na password zao, na pia watapata mapendekezo binafsi ya filamu na michezo ya kuigiza.

Je, umeridhika na Netflix kuongeza gharama kwa kuchangia password?

 

Mwandishi Emmanuel Tadayo Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
mwandishi wa habari za teknolojia kwenye tovuti pendwa ya mtaawasaba
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive