hapa siongelei kibajaji, wala kampuni yoyote ya kichina naongelea kampuni kubwa kabisa ya magari inayoiitwa Volkswagen ambao wametengeneza hili gari One litre car.
hili gari linaingia watu wawili na limetengenezwa kwa kutumia vitu vyepesi ili kulifanya kutumia mafuta kidogo sana aina ya diesel hadi kufikia kutembea umbali wa kilomita 100 kwa kutumia lita 1 tu ya mafuta.
mwezi huu wa pili volkswagen wamethibitisha kua kuanzia mwaka huu wataanza kutengeneza haya magari kwa ajili ya wateja baada ya kukaa muda mrefu kama concept tu. je lakini hili gari limeanzia wapi
safiri dar mpaka arusha kwa lita saba tu
prototype kuanzia mwaka 2002
ilikua mwaka 2002 hii idea ilipoanza na kuanza kuunda concept walitumia vitu vyepesi kama body la carbon fiber (plastic imara na jepesi) wakatumia na vitu vya alluminium kama vile breki ili gari liwe jepesi. na mpaka linakamilika lilikua na uzito wa kilogram 290 tu na kilikua na power ya one cylinder 299cc. je kama mtu anabeba magunia mawili angeshindwa kukibeba hiki kigari?.  habari iliendeleaa wee mwaka 2007 wakasema kitakua tayar by the end of decade (2010) na bei itakua million 40 hadi 60 ya kitanzania. lakini mambo hayakua tena.
mwaka 2009 wakakatengeneza kengine
ilipofika huu mwaka wakamodify kingine na kuachana na kile cha mwanzo. hiki walikipa jina L1 na waliendelea na concept ile ile ya watu wawili  hiki kiliongezeka uzito na kufikia kilogram 381 na power ikaongezwa kua two cylinder 800 cc. Wenyewe volkswagen waliclaim kinaweza kutembea speed hadi 158km kwa saa moja na speed ya kuanzia 0km/hr hadi 100km/hr inaweza fikiwa kwa sekunde 14 tu (speed ya kuvuta mafuta).
mwaka 2011 kikaimprove zaidi
hapa walikibadili jina na kukiita xl1 na wenyewe volkswagen wakasema hii gari limeiprove zaidi na litakula mafuta 0.9 litre kwa kila kilomita 100 na lina uwezo wa kutembea hadi km 35 bila mafuta kwa kutumia nguvu ya umeme tu. gari likazidi kuongezeka uzito kufikia kilogram 795. speed ilibaki pale pale 158km kwa saa 1 lakini speed ya kuvutia mafuta ikaongezeka likawa linaweza kutembea kilomita 0/hr hadi 100/hr kwa sekunde 11 tu.
boom la mwanachuo 7500 linatosha kuhudumia hii gari
bei itatangwazwa mwezi ujao kwenye maonesho ya magari geneva huko uswiss
mwezi huu februari wamesema gari lao lipo tayari sasa na kuanzia mwisho mwaka huu litaanza kuuzwa. japo machache tu yametengenezwa lakini yatauzwa mwaka huu. na ule mwendo wa kutembea na umeme bila mafuta umeongezeka hadi km 50 so gari likiisha mafuta njiani hupati shida unatumia umeme kwa kilomita 50.
tuandikie @mtaawasaba