OnePlus 5T: Unahitaji simu hii kwa matumizi zaidi ya simu

Diana Benedict Maoni 148

OnePlus 5T

Simu ya OnePlus 5T ilizinduliwa mnamo Novemba 2017. Simu inakuja na kionyesho cha skrini ya inchi 6.01 na Resolution ya pixels 1080 na pixels 2160 kwenye PPI ya saizi 401 kwa inchi.

OnePlus 5T 1

OnePlus 5T inaendeshwa na processor ya octa-core ya Qualcomm Snapdragon 845 ya 2,45GHz na inakuja na 6GB/8GB ya RAM. Paki ya simu ni 64GB/128GB katika hifadhi ya ndani ambayo haiwezi kupanuliwa (Non-Expandable). Mbali na hayo, OnePlus 5T ina kamera mbili za nyuma zenye megapixel 20 na megapixel 16 ya wide angle, kamera ya mbele ina megapixel 16 kwa selfies.

OnePlus 5T 2

OnePlus 5T inaendeshwa na Program ya Android 7.1.1 Nougat ambayo unaweza ku upgrade mpaka Android 8.1 Oreo na inatumiwa na betri isiyoondolewa ye ukubwa wa 3300mAh. Inachukua ukubwa wa 156.10 x 75.00 x 7.30 (urefu x upana x uzani) na uzito wa gramu 162.00.

OnePlus 5T ni smartphone inayotumia SIM (GSM) mbili ambayo inakubali Nano-SIM kwa pande zote mbili. OnePlus 5T ina viunganishi vya Wi-Fi, GPS, Bluetooth, NFC, USB OTG, 3G na 4G (LTE). Sensor za kwenye simu ni pamoja na Magnetometer Compass, Proximit Sensor, Accelerometer, Sensor ya kupunguza na kuongeza mwanga na Gyroscope.

oneplus 5t sandstone white 6

muonekano

Nimependa sana umbo la OnePlus 5T yenye aluminium, ingawa ni sawa na toleo la nyuma yake OnePlus 5. Mipaka ya simu na Kioo ni mizuri na sio kubwa sana na ni nyembamba sana.

Tofauti na OnePlus 5, 5T hupatikana pia katika rangi nyeupe na uzuri wa simu hii ni kwamba fingerprint scanner ya sasa iko chini kamera ya nyuma, badala ya mbele ya simu kama models zilizopita.

OnePlus5T001 1

hitimisho

Simu ya OnePlus 5T inapatikana kwa Dola za kimarekani 600$ ambayo ni bei rahisi ukilinganisha na Simu za Samsung na iPhones.

endelea kuwa nasi kwa kutufuata kwenye mitandao ya kijamii. pia usiache ku comment, like na ku sbscribe kwenye channel yetu ya youtube

 

Mwandishi Diana Benedict Mwandishi
Mitandao ya Kijamii
Diana Benedict. Digital Creator | IT Specialist | Graphics Designer | Web Designer | Web SEO | Contents Management | UI/UX Designer and Social Media Management.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive