Katika onesho la pili la Galaxy Unpacked la mwaka huu, #Samsung imerudisha rasmi mduara unaozunguka kwenye saa janja mpya iliyozinduliwa leo ya Galaxy Watch 6 Classic. Saa janja hii inakuja katika ukubwa sawa wa 43mm na 47mm kama sawa na toleo la awali ( Watch 4 Classic), pia inakuja ikiwa imefunikwa na chuma cha pua. Pia imezindua simu zinazojikunja za Galaxy Fold 5 na Flip 5, pamoja na tableti.
ukiachana na Watch 6 Classic, Samsung ilizindua Galaxy Watch 6 ya kawaida, ambayo kampuni imeleta katika ukubwa wa 40mm na 44mm ikiwa imefunikwa na alumini. Saa zote mbili zina vioo imara kutoka kwene madini ya sapphire na ukubwa kidogo kuliko mtangulizi. Pia zinakuja na toleo jipya kabisa la mfumo endeshi wa Wear OS 4 na One UI 5, ambayo itaweza kutoa taarifa mbalimbali ukiwa umelala, taarifa za mapigo ya moyo, simu za dharula na mengine mengi.
Saa janja ya Watch 6 Classic itagharimu dola za marekani 400 itakapoingia sokoni, wakati Watch 6 ya kawaida ina bei ya dola za marekani 300.