Leo Tarehe 25 Februari 2018 katika Maonesho ya Simu ya MWC Kampuni ya Samsung imezindua Simu mbili mpya Samsung Galaxy S9 na Samsung Galaxy S9+ plus. Mtaawasaba imefanya uchambuzi wa kina katika simu hizi mbili na kukuletea sifa, muonekano, bei na vitu vipya vilivyoongezeka katika simu hizi mbili.
Muundo na kioo
Samsung Galaxy S9 na S9 Plus zimeundwa kwa Aluminum pembeni yake na yenye umbo la kioo kigumu katika shepu yake ya nyuma, Ukilinganisha toleo la Samsung S8 Na S8 Plus halina tofauti sana katika umbo lake la mbele, Tofauti kubwa iliyopo ni katika umbo la nyuma hasa katika Fingerprint reader zake na kamera.
Samsung Galaxy S9 ina uzito wa gramu zisizopungua gramu 163 na umbo la milimita mstatili wa 147.7mm Urefu, 68.7mm Upana, wembaba wa 8.5mm na ukubwa wa kioo wa inchi 5.8 Super AMOLED na Samsung Galaxy S9 Plus ina uzito wa gramu zisizopungua gramu 189 na umbo la milimita mstatili wa 158.1mm Urefu, 73.8mm Upana, wembaba wa 8.5mm na ukubwa wa kioo wa inchi 5.8 Super AMOLED, Pia simu hizi zinalindwa na kizuizi cha maji cha IP68.
Kamera
Tofati kubwa niliyoiona imeongezewa katika simu hizi mbili ukilinganisha na toleo la mwaka uliopita la Samsung S8 na S8 Plus, kimojawapo ni mabadiriko makubwa katika camera.
Tukianza na Samsung Galaxy S9 yenyewe ina Super Speed Dual Pixel camera ya nyuma yenye 12MP (megapixel) AF sensor ikiwa pamoja na OIS F1.5 hadi F2.4 appecture yenye uwezo wa kupiga picha hata kwenye mwanga hafifu ukapata picha nzuri yenye quality, Ni kweli kwamba wingi wa pixel sio kitu kwenye camera lakini lens iliyowekwa kwenye camera hii ya Samsung S9 inayofunga na kufunguka kutokana na mwanga hafifu au mkali uliopo. Kwa upande wa camera ya mbele Samsung Galaxy S9 ina ukubwa wa Megapixel 8.0MP yenye AF (F1.7) kwa ajili ya selfie na video recording.
Tukija kwa Samsung Galaxy S9 Plus ina kamera Mbili (Dual Camera) yenye Dual OIS / Wide-angle: Super Speed Dual Pixel 12MP AF sensor (F1.5/F2.4), Telephoto: 12MP AF sensor (F2.4) ambayo inasupport low lingt, inayokupa picha za wide angle na kamera ya mbele nyenye Megamixel 8.0MP ambayo haina tofauti na ya S9.
Tofauti kubwa imefanyika katika kamera za simu hizi mbili ambayo zinaweza kufanya animation ya sura yako, ambayo utaweza kurekodi video fupi ukamtumia mpendwa wako.
Teknolojia ya Sauti
Simu hizi mbili zinakuja na mfumo ulioboreshwa kabisa wa sauti ambapo zitakuwa na spika za stereo iliyochujwa na AKG. Ambayo inatoa sauti kubwa kwa sailimia 40 zaidi ya mtangulizi wake Galaxy S8,
Mfumo endeshi , Betri na ufanyaji kazi
Simu zote mbili zinakuja na toleo jipya kabisa la Android: 8.0 Oreo. Kama ilivyo jadi ya Samsung mfumo endeshi umefunikwa na ngozi maarufu kama Samsung Experience pia simu hizi app kwa ajili usaidizi Bixby ambayo ilianza kuonekana kwenye simu zilizotoka mwaka jana. Bixby ambayo kwa sasa imezidi kuerevuka, inaweza kutafsiri lugha za kigeni muda huohuo na kupitia kuangaza kamera.
Simu ya Galaxy S9 inatumia prosesa ya Qualcomm Snapdragon 845 kwa simu zitakazouzwa Marekani na China wakati kwa nchi zingine zilizobaki simu zitakuwa na prosesa inayotngenezwa na Samsung wenyewe ya Exynos 9810. Galaxy S9+ inakuja na RAM ya 6GB na ukubwa wa hifadhi wa 128GB wakati kwa upande S9 hakutakuwa na mabadiliko yoyote kwa mtangulizi wake ambapo itakuwa na RAM ya 4GB na hifadhi ya ndani 64GB.
Samsung Galaxy S9 and Samsung Galaxy S9 Plus hazina mabadiliko yoyote kwenye upande wa betri ambapo betri zina ukubwa wa 3,000mAh kwa Samsung Galaxy S9 na 3,500mAh kwa Samsung Galaxy S9 Plus , ambao ni ukubwa sawa na watangulizi wao Galaxy S8 and Galaxy S8 Plus.
Sifa za Samsung Galaxy S9 na Samsung Galaxy S9+
Unaweza kuona Specification zote za simu hizi mbili kupitia chati hii:
Samsung Galaxy S9 | Samsung Galaxy S9 Plus | |
---|---|---|
Kioo | kioo kilichojikunja chenye 5.8-inch teknolojia ya Super AMOLED (Quad HD+) 570 ppi uwiano wa picha ni 18:5:9 | kioo kilichojikunja chenye 6.2-inch teknolojia ya Super AMOLED (Quad HD+) 529 ppi uwiano wa picha ni 18:5:9 |
Prosesa | nchi zingine: 10 nm, 64-bit, octa-core Samsung Exynos 9810 (2.8 GHz quad + 1.7 GHz quad) marekani: 10nm, 64-bit, octa-core Qualcomm Snapdragon 845 | nchi zingine: 10 nm, 64-bit, octa-core Samsung Exynos 9810 (2.8 GHz quad + 1.7 GHz quad) marekani: 10nm, 64-bit, octa-core Qualcomm Snapdragon 845 |
GPU | ARM Mali-G72 (Exynos) Adreno 630 (Snapdragon) | ARM Mali-G72 (Exynos) Adreno 630 (Snapdragon) |
RAM | 4 GB | 6 GB |
Hifadhi/Ujazo | 64 / 128 / 256 GB inaweza kuongezwa mpaka 400 GB | 64 / 128 / 256 GB inaweza kuongezwa mpaka 400 GB |
Kamera | nyuma: Super Speed Dual Pixel 12 MP AF sensor with OIS, f/1.5 and f/2.4 apertures mbele: 8 MP AF sensor, f/1.7 aperture | nyuma: Dual camera with dual OIS ncha pana: Super Speed Dual Pixel 12 MP AF sensor with OIS, f/1.5 and f/2.4 apertures Telephoto: 12 MP AF sensor, f/2.4 aperturembele: 8 MP AF sensor, f/1.7 aperture |
Betri | 3,000 mAh isiyoweza kutoka Fast Wired Charging yenye QC 2.0 Fast Wireless Charging yenye WPC na PMA | 3,500 mAh isiyoweza kutoka Fast Wired Charging yenye QC 2.0 Fast Wireless Charging yenye WPC na PMA |
Mtandao | Enhanced 4X4 MIMO / CA, LAA, LTE Cat. 18 | Enhanced 4X4 MIMO / CA, LAA, LTE Cat. 18 |
Muunganiko | Wi-Fi 802.11 a/b/g/n/ac (2.4/5 GHz) VHT80 MU-MIMO 1024QAM Bluetooth v5.0 (LE up to 2 Mbps) ANT+ USB Type-C NFC Location: GPS, Galileo, Glonass, Beidou | Wi-Fi 802.11 a/b/g/n/ac (2.4/5 GHz) VHT80 MU-MIMO 1024QAM Bluetooth v5.0 (LE up to 2 Mbps) ANT+ USB Type-C NFC Location: GPS, Galileo, Glonass, Beidou |
Sensa | Iris Pressure Accelerometer Barometer Fingerprint Gyro Geomagnetic Hall HR Proximity RGB Light | Iris Pressure Accelerometer Barometer Fingerprint Gyro Geomagnetic Hall HR Proximity RGB Light |
Ulinzi | Lock type: pattern, PIN, password Biometric lock type: iris scanner, fingerprint scanner, face recognition, Intelligent Scan | Lock type: pattern, PIN, password Biometric lock type: iris scanner, fingerprint scanner, face recognition, Intelligent Scan |
Teknolojia ya sauti | Stereo speakers tuned by AKG, surround sound with Dolby Atmos technology Audio playback format: MP3, M4A, 3GA, AAC, OGG, OGA, WAV, WMA, AMR, AWB, FLAC, MID, MIDI, XMF, MXMF, IMY, RTTTL, RTX, OTA, APE, DSF, DFF | Stereo speakers tuned by AKG, surround sound with Dolby Atmos technology Audio playback format: MP3, M4A, 3GA, AAC, OGG, OGA, WAV, WMA, AMR, AWB, FLAC, MID, MIDI, XMF, MXMF, IMY, RTTTL, RTX, OTA, APE, DSF, DFF |
Video | MP4, M4V, 3GP, 3G2, WMV, ASF, AVI, FLV, MKV, WEBM | MP4, M4V, 3GP, 3G2, WMV, ASF, AVI, FLV, MKV, WEBM |
Uwezo wa Virtual reality | Gear VR with controller (SM-R325NZAXAR) Google Daydream View | Gear VR with controller (SM-R325NZAXAR) Google Daydream View |
Mfumo endeshi | Android 8.0 Oreo | Android 8.0 Oreo |
Upana na uzito | 147.7 x 68.7 x 8.5 mm 163 g | 158.1 x 73.8 x 8.5 mm 189 g |
Rangi | Midnight Black, Coral Blue, Lilac Purple, Titanium Grey | Midnight Black, Coral Blue, Lilac Purple, Titanium Grey |
Picha
Vitu vingine
Simu hizi mbili zinakuja na emoji kama za kwenye iPhone X walizojipa jina la AR Emoji. Ambayo inachukua taswira ya uso wako na kutengeneza avatar ya 3D inayofanana na wewe kama kwenye iPhone X
Pia Simu hizi mbili zinaweza kupachikwa kwenye DeX pad ambayo ni maboresho ya kifaa kinachoweza geuza simu kuwa na muonekano wa kompyuta ambao utakuwezesha kufanya kazi kwenye monitor kubwa kama ambavyo unatumia kompyuta wakti huo simu ikiendelea kujichaji.
Bei, Upatikanaji na neno la mwisho
Samsung Galaxy S9 Inatarajiwa kuuzwa kati ya Dola za kimarekani 720 sawa na Sh 1,658, 000/= tzs na Samsung Galaxy S9 Plus inatarajiwa kuuzwa kati ya dola za kimarekani 840 sawa na Sh, 1,955,000/= tsh, Japo hizi ni bei za kampuni za kimarekani haijathibishishwa kwa Tanzania Zitauzwa Shilingi ngapi.
Kwa huku kwetu hatujajua bado simu hizi zitaanza kupatikana kuanzia lini lakini kwa ulaya zitaanza kuingia sokoni kuanzia marchi 16 mwaka huu huu.
Tupe maoni yako kuusu na simu hizi mbili kwenye sehemu ya comment hapo chini. Pia Endelea kuwa nasi kujua zaidi kuhusu uchambuzi wa simu na mambo mengine ya teknolojia, Pia usisahau kutufollow kwenye mitandao ya kijamii kama Twitter, facebook na Instagram.
Kuna tofauti gani kati ya samsung s8 na s8 plus?