Uchambuzi wa iPhone 14 Pro na 14 Pro Max: Karibu kwenye Dynamic Island

Simu mpya za Apple pia zinakuja na kamera zilizoboreshwa, kichakataji chenye kasi zaidi, skrini inayowashwa kila wakati na iOS 16 bila kusahau vipengele vipya vya usalama ikiwa ni pamoja na Crah detection na SOS ya Dharura kupitia Satellite.

Diana Benedict Maoni 152
Apple Event 2022: iPhone 14, Apple Watch Series 8 na kila kitu kilichotangazwa
9.3 Neno la Mwisho
iPhone 14 Pro na 14 Pro Max
2,800,000 TZS

Simu za iPhone 14 Pro na Pro Max zinaweza kuonekana sawa na iPhone 13 Pro ya mwaka jana, lakini usiruhusu hilo likudanganye. Tofauti kubwa iko kwenye kioo cha iPhone 14 Pro ambapo kuna kitu kipya kinachoendelea. Kwa mara ya kwanza Apple wanaondoa Notch kiengele maarufu ambacho ndicho kimekuwa kama utambulisho wa simu hizi za Apple toka mwaka 2017, badala yake wamezindua kipengele kipya kilichopewa jina la Dynamic Island. Kipengele hiki mithili ya kidonge kimekatwa kwenye kioo na kipengele hiki kinashikilia mfumo wa kamera ya TrueDepth iliyoboreshwa. Kipengele hiki cha Dynamic Island kinaleta fursa zingine kutoa taarifa mbalimbali za mfumo ambazo hazikuwapo awali kwenye kipengele cha Notch. Pamoja na maboresho haya, tupitie sifa mbalimbali za hizi simu mbili.

Dynamic Island

iphone 14 pro dynamic island 1
kwa hisani ya CNET

Kama tulivyoelezea kwa ufupi hapo juu kipengele hiki kipya. Dynamic Island ni kisiwa cha ajabu kinachoitwa kinachofafanua simu hizi mbili. Kadiri muda unavyotumia hizi simu mbili, ndivyo unavyozidi kuelewa zaidi kuhusu kipengele hiki kipya. Inafanya kazi katika hali nyingi na ni njia rahisi ya kuona kinachoendelea bila kuvuta umakini wako mbali kabisa na kile unachofanya.

Always-on display

always on iphone 14 pro

The iPhone 14 Pro inakuja na mfumo endeshi wa iOS 16, mfumo huu unakuja na vipengele vipya vya kuvutia kama vile uwezo wa kubadili na kubinafsisha lock screen. Kuna kipengele kimoja kilichowekwa mahususi kwa ajili ya simu za 14 Pro na 14 Pro Max ambacho ni always on display.

Always on display ni mfumo unaotumia umeme kidogo ili kukupa taarifa mbalimbali kwenye skrini yako bila kubonyeza simu. Kwa watumiaji wa simu zinazotumia mfumo endeshi wa android kipengele hiki sio kigeni kwani kimekuwepo kwa muda sasa.

Kwenye simu za 14 Pro kipengele hiki kinaonesha taarifa mbalimbali ikiwemo muda, siku, wijeti , na taarifa zingine. Kutegemeana na lock screen yako ilivyopangwa, always on display inaweza kutofautiana kati ya simu na simu. 

Muundo na kioo

Muundo wa simu hizi mbili unafanana kwa karibu sana na watangulizi wake, kwa upande mmoja zinafanana sana na iPhone 13 Pro isipokuwa upande wa nyuma kamera ni kubwa na zilizojitokeza zaidi kuliko watangulizi. Kwa kifupi Apple hawajataka kujibidiisha sana kwenye upande huu wa maboresho.

iphone 14 pro muundo nyuma

Kwa upande wa mbele ya simu hizi mpya za Apple inaonekana tofauti sana. Notch imeondoka, nafasi yake imechukuliwa na Dynamic Island chenye umbo la kidonge. Muundo wa zamani wa iPhone uliochoka hatimaye umepata maboresho, ingawa mkato bado ni mkubwa kuliko ule ulio kwenye simu bora za Android.

iphone 14 pro muundo mbele

Simu za IPhone 14 Pro zimezungushiwa fremu ya chuma cha pua na kuwekwa kioo cha nyuma chenye muonekano usio wakuteleza yenye muundo rahisi. Kioo kimewekewa teknolojia ya  Ceramic Shield kwa ajili ya kutoa uimara wa ziada. Muonekano wa kamera za nyuma ni mkubwa uliojitokeza zaidi unaoifanya simu ishindwe kukaa kwenye uso wa tambarare, japo unaweza kuondokana na tatizo hili kwa kuiwekea kava simu yako.

Kwa upande wambele hakuna mabadiliko makubwa zaidi ya kuondolewa kwa notch na kuongezwa Dynamic Island ambayo tayari tumeielezea hapo juu.

Kioo cha simu hizi kimetengenezwa na Samsung, na ndicho kinaaminika ndio kioo bora zaidi na angavu kuliko vioo vya simu zote kwa sasa. Kioo hiki kinakuja na teknolojia ya Promotion na kinakuja na uwezo wa 120Hz ambazo hushuka hadi 1Hz simu inapokuwa haitumiki ili kuweza kuongeza maisha ya betri.

Kamera

iphone 14 pro kamera

Simu hizi mbili zina kamera 3 kwa upande wa nyuma, kamera kuu ni wide angle, ingine ni ultra wide na ingine ni telephoto yenye uwezo wa optical zoom hadi mara tatu zaidi. Kamera kuu inakuja na sensa yenye megapikseli 48. Sensor ya ultrawide ya 12MP pia iliona kuongeza na sensor mpya ambayo ni kubwa mara mbili zaidi ya ile kwenye iPhone 13 Pro. Lenzi ya telephoto bado ni 3x.

Kamera ya selfie kwenye iPhone 14 Pro inakuja na maboresho kadhaa, pia. Autofocus sasa inakuja imeboreshwa, kipengele ambacho nimekuwa nikitaka kuona kwa muda sasa. Apple inasema aperture ya kamera ya TrueDepth itahakikisha selfie bora za mwanga mdogo. Kamera inayoelekea mbele pia inapata ufikiaji wa Injini ya Photonic. 

 

Apple Event 2022: iPhone 14, Apple Watch Series 8 na kila kitu kilichotangazwa
iPhone 14 Pro na 14 Pro Max
Neno la Mwisho 9.3
Kasi ya iPhone 14 Pro 10 out of 10
Betri ya iPhone 14 Pro 8 out of 10
Kamera 10 out of 10
Mwandishi Diana Benedict Mwandishi
Mitandao ya Kijamii
Diana Benedict. Digital Creator | IT Specialist | Graphics Designer | Web Designer | Web SEO | Contents Management | UI/UX Designer and Social Media Management.
Leave a review
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive