Kipindi kichache kilichopita WhatsApp ilizindua Programu yao mpya ya WhatsApp Business inayowawezesha wafanya Biashara wadogo wadogo kuweza kuendesha Biashara zao kupitia mtandao huo wa WhatsApp. Leo nimekuletea Baadhi ya vipengele vipya ambavyo havipatikani kwa mtumiaji wa whatsapp ya kawaida;
Kuacha Ujumbe Pale unapokuwa uko mbali na Simu.
Japo sio kitu kipya katika mitandao ya kijamii ikiwepo Facebook Messenger ndio ilianzisha huduma hiyo ya kuacha ujumbe mfupi (Welcome Message). Kipengele hiki kinaweza kukufanya uweze kuset aina ya ujumbe unaotaka umfikie mteja wako pale anapokutumia ujumbe na kuweza kumjibu papo hapo utakapokuwa uko mbali na simu yako.
Wasifu wa Biashara
Kwa kutumia WhatsApp Business utaweza kuweka wasifu wa biashara yako na maelezo mengine ya Biashara inapopatikana na kazi unazozifanya na website ya biashara yako
Kudhibiti Miamala
Whatsapp Business inakuwezesha kudhibiti miamala ya wateja wako kwa kutambua mteja mpya, mteja aliyelipa na mteja ambaye bado hajalipa katika biashara hiyo.
Kwa sasa Programu ya Whatsapp Business inapatikana kwa simu za Android tu unaweza ipakuwa hapa
Tufuatilie kwenye mitandao mbali mbali ili usipitwe na Habari, Uchambuzi naMakala mbali mbali ya mitanadoni na ya kiteknolojia kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Google+ na Youtube, Pia usisite kutoa maoni yako hapo chini au tuandikie barua pepe kwa [email protected]
Kuna mpango wowote wa malipo kwa huduma hii?
hapana, huduma ya whatsapp business ni free kwa sasa, bado hawajatangaza kama kuna mpango wowotw wa malipo kuhusu huduma hii
Umetisha mzee baba kwa habari big up